Kuisaka mizizi ya familia zaidi ya DNA

Get monthly
e-newsletter

Kuisaka mizizi ya familia zaidi ya DNA

Wataalam watatu wa unasaba wanavifafanua vikwazo na mafanikio katika kutafiti ukoo wa Wamarekani Waafrika
Afrika Upya: 
18 January 2024
Photos of Dena M. Chasten (on the beach)
Dena M. Chasten (supplied)
Dena M. Chasten amesimama ufukweni. Alipata wazazi wake waliomzaa na sasa anafanya kazi kama mtaalamu wa nasaba akiwasaidia Waamerika wengine wa Kiafrika katika kurekebisha matawi yaliyovunjika ya miti ya familia zao.

Akiwa mtoto wa kupangwa, Dena M. Chasten mara nyingi alihisi kutengwa na familia yake. Hisia hiyo inahusiana na tajriba yake ya kuwa Mmarekani Mwafrika huko Marekani. Kila mara aliwazia alikotoka na alikostahili.

"Tofauti ni kwambaanapokuwa umepangwa, kwa kiasi kikubwa, huwa unatakiwa. Nilikuwa na bahati sana kwamba familia nzuri ilinilea,” alisema mzaliwa huyo wa Philadelphia. “Hata nilifanana nao, lakini nilijua kabisa kwamba hatukuwa na uhusiano wa kinasabai. Bado nilijihisi nimepotea.”

Tajriba hiyo ilimtia moyo Bi. Chasten sio tu kuwasaka wazazi wake kibayolojia bali pia kuuchunguza ukoo wake. Alianza uchunguzi wa kinasaba na ukoo ambao uliyazua maswali mengi kuliko majibu.

Katika eneo lote la katikati mwa Atlantiki, Bi. Chasten ameshiriki safari yake katika maktaba, jamii za kihistoria na hata katika Makavazi ya Kitaifa ya Smithsonian ya Historia na Utamaduni wa Wamarekani Waafrika huko Washington, DC.

Kwa kuwa sasa amewapata wazazi wake waliomzaa, anafanya kazi kama mtaalamu wa unasaba, akiwasaidia Wamarekani Waafrika wengine katika kuurekebishauhusiano wao wa kinasaba uliovunjika.

Ushahidi wa stakabadhi

"Mfumo wa utumwa ulizitenga familia, lakini DNA huziunganisha familia hizo," alisema Nicka Sewell-Smith, mtayarishaji mkuu wa hadithi wa  Ancestry.com.

Nicka Sewell-Smith
Mfumo wa utumwa ulizitenga familia, lakini DNA iunaziunganisha famila hizo.
Nicka Sewell-Smith
Mzalishaji Mkuu wa Hadithi, Ancestry.com

Watu hawapaswi kutegemea tu DNA (Asidi DeoksiriboNukleini), alisema. "Wale ambao tumezama katika taaluma ya unasaba tunataka kupata ushahidi wa stakabadhi ili kuifanya miunganisho hiyo.”

Kwenye makala ya Finding Your Roots na Henry Louis Gates Jr., watazamaji wanawafuatilia Wamarekani Waafrika wengi huku wakisaka ukoo wao hadi kwa mababu zao waliokuwa watumwa. 

“"Wamarekani Waafrika walikabiliwa na kikwazo cha kipekee cha kinasaba katika miaka hiyo 10 hadi 20 ya kwanza kutoka utumwani na Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe," Nick Sheedy, mtaalamu mkuu wa unasaba katika kipindi hicho.“ "Sensa ya 1870 ni sensa ya kwanza ya kitaifa ambayo ilimworodhesha kila mtu kwa jina," Bw. Sheedy aliiambia Africa Renewal katika mahojiano, akiongeza kuwa majina hayo yangebadilikakutegemea umiliki, uchaguzi wa kibinafsi na sababu nyingine zisizoweza kuelezeka.

Kufuatilia mizizi ya Waafrika waliokuwa watumwa, ambao walichukuliwa kuwa mali, kwa kawaida kulihitaji kuangalia mauzo ya mirathi, rekodi za mirathi, hati za kodi na hatimiliki, Bw. Sheedy alieleza. Wakati wa Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe, aliongeza, askari walizichoma mahakama za kaunti ambazo zilikuwa na kumbukumbu nyingi za enzi ya watumwa.

"Hakuna orodha kuu ya Waafrika waliofanywa watumwa," alisema Bi. Sewell-Smith.

Ingawa rekodi nyingi haziko mtandaoni, alibainisha kuwa hati milioni 3.5 kutoka Ofisi ya Freedmen— ambazo sasa zinapatikana kwenye Ancestry.com — ni mahali pazuri pa kuanzia.

Mojawapo ya mafanikio ya ushahidi wa stakabadhi wa Bw. Sheedy yalihusiana na Ahmir "Questlove" Thompson, mpiga ngoma kutoka bendi ya hip-hop inayoitwa The Roots.

"Tuligundua kuwa mababu zake walikuja kwenye Clotilda," Bw. Sheedy alisema. Ilikuwa meli ya mwisho inayojulikana ya watumwa kuwasili Marekani.” 

Nick Sheedy, Lead Genealogist, Finding Your Roots with Henry Louis Gates, Jr.
Sote tunahusiana.
Nick Sheedy
Mtaalam Mkuu wa Unasaba, Finding Your Roots with Henry Louis Gates, Jr.

Ulinganifu wa DNA 

Bi. Sewell-Smith anapoufichua ukoo wake mwenyewe, hafuatilii asili yake katika nchi moja ya Kiafrika; anaandama bara zima. "Ni Lazima uzingatie ni vizazi vingapi vilikuwepo tangu kupiga marufuku mwaka 1808 kwa uingizaji wa watumwa kutoka Afrika," alisema.

Kuhesabu vizazi sita kurudi nyuma kunahusisha kufuatilia mizizi ya mababu na mababu 64 kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika.

Bi. Sewell-Smith anaonya kwamba watu hukosa uhakika ikiwa wanazingatia nchi au asilimia. "Kwa Wamarekani Waafrika, asili zetu zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinatoka katika maeneo mengi," alisema. “Ninajua ‘wapi’ . Ninataka kujua ‘nani’.”

Katika familia ya Bi. Sewell-Smith, "nani" ni pamoja na bibi yake mwenye umri wa miaka 99, ambaye babu na babu walikuwa watumwa. 

"Bibi yangu anashiriki 30 centimorgans za DNA na mwanamke wa Naijeria ambaye ni kizazi cha kwanza katika familia yake kuzaliwa Marekani," alisema. "Huyo ni binamu wa nne!"

Watu wanaufanya uvumbuzi huu kila siku, alisema.

Hata Bw. Sheedy anaweza kuipata mizizi yake katika bara hilo. “Bibi yangu, Betty alikuwa mweupe hasa na nywele za kimanjano na macho ya buluu. Mababu zake wote walikuwa waanzilishi wa California, na alikuwa na karibu asilimia tatu ya DNA ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara," alisema. "Sote tunahusiana."

Wataalamu wa unasaba wanaweza kutatua mafumbo zaidi ikiwa watu wengi watapima DNA, alisema Bi. Sewell-Smith.

"Uwezo uko kwenye ulinganifu wa DNA," aliongeza. Hiyo ndiyo itasimulia hadithi, kutupa vidokezo, kututuma kwenye hifadhi za nyaraka na kutuunganisha na watu ambao hatungejua kuwa walikuwa jamaa zetu.

Binamu wa mbali

Huku akisubiri matokeo ya vipimo kadhaa vya DNA, Bi Chasten alisema anatarajia kubaini mahali ambapo angeweza kuwakilisha. "Nilikuwa ninaenda kutafuta nchi yangu na kuwa na uhusiano wangu."

Dena M. Chasten, genealogist
You can’t depend just on the DNA. You have to do the research.
Dena M. Chasten
mtaalam wa unasaba

Badala yake uchunguzi wake wa mitochondria ulifichua kwamba babu yake mkubwa wa kuukeni alikuwa mwanamke wa Ulaya, na uchunguzi wake wa kiautosom ulionyesha asilimia ya DNA kutoka kanda za pande zote nne kuu za bara hilo.

Akiwa amestaajabu na kuchanganyikiwa, Bi. Chasten alisema alikuwa na maswali zaidi kuliko hapo awali. Wakati huu, hata hivyo, alijua ni wapi pa kuangalia. "Huwezi kutegemea tu DNA," alisema. "Ni lazima uufanye uchunguzi, ili yote yawe na maana."

Bi. Chasten aliupata ulinganifu thabiti wa DNA nchini Ghana, nchi iliyobeba asilimia zake kubwa zaidi. Aliwasiliana na binamu huyu wa mbali na akasikia hadithi ambayo ingali inampa msisismko.

"Kulikuwa na mighani kwamba nyanya yake [binamu wa Ghana] angenda kulala kila mara akiomba msamaha kwa sababu alijua jukumu la mababu zake katika biashara ya utumwa," Bi. Chasten alisema. "Kilikuwa kitu ambacho alihitaji kulipia."

Hadithi hiyo iliibua hisia zinazokinzana kwa Bi. Chasten: hangeweza kuyakubali matendo ya mababu zake alipokuwa akimfariji binamu yake.

“Nilimwambia, ‘Usijali kuhusu hilo. Tunarejea. Siwezi kueleza kilichotokea wakati huo, lakini sasa tuyanarekebisha.’ Kwa hiyo wengi wetu tunarejea nyumbani.”

Bi. Chasten alilizuru bara hilo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana.