Bingwa wa Mifumo ya Chakula Lucy Muchoki, Kenya

Get monthly
e-newsletter

Bingwa wa Mifumo ya Chakula Lucy Muchoki, Kenya

Mkurugenzi Mtendaji, Pan-African Agribusiness and Agroindustry Consortium (PanAAC) imeandaa mazungumzo kwa Afrika Kusini katika eneo la SMEs.
Franck Kuwonu
9 June 2021
.
Lucy Muchoki
Lucy Muchoki

Je, inahisije kuwa Bingwa wa Chakula wa Umoja wa Mataifa?

Inapendeza sana! Inaridhisha sana kutambuliwa kama 'bingwa' kwa sababu ya kazi yangu. Na sio kazi yoyote tu, lakini kitu ninachopenda kukifanya! Imenifanya nitambue kuwa mtu anapaswa kustawi na kuendelea kufanya kile anachoamini na kukifanya vizuri, na kwa shauku na bidii. Kuna mtu mahali fulani atazingatia na kutambua juhudi zako.

Tangu nilipoteuliwa kama Bingwa wa Chakula, nimekutana na watu tofauti na nikasikiliza maoni mengi ya kiubunifu, ya kuvutia mawazo kuhusu jinsi ya kuimarisha na kusaidia mifumo yetu ya chakula. Imekuwa tajriba nzuri. Kupitia uteuzi huu, nimekutana  na karibu kila mtu niliyehitaji kujua katika sekta ya chakula kote ulimwenguni.

Majadiliano haya mengi yanapita mikutano kwa mtandao ambayo huratibiwa na Umoja wa Mataifa. Kuna mawasilisho mengi na maoni halisi ya kiubunifu tunayoshikilia kutoka pande zote.

Kama mwanamke wa Kiafrika, najisikia kuheshimiwa kuwa miongoni mwa mabingwa hawa wakuu wa chakula wanaoshikilia matumaini ya bara hili. Ninaona safari ambayo tumeanza pamoja na nina matumaini zaidi kuwa tuko njiani kufikia Azimio la Malabo [Azimio kuhusu Ukuaji wa Haraka wa Kilimo na Mageuzi ya Ustawi wa Pamoja na Kuboreka kwa Njia za Utafutaji riziki kunakothibitisha dhamira kuu ya nchi za Afrika kutenga 10 % ya rasilimali za umma kwa kilimo].

Je,  ulianza utetezi kuhusu chakula lini?

Kwa muda mrefu zaidi, nimekuwa nikitetea msaada na maendeleo ya wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) katika sekta ya chakula. Afrika ina uwezo wa kukua na kujilisha. Biashara zetu ndogondogo za chakula  ndizo tumaini la mageuzi yetu ya kiuchumi na maendeleo.

Nimekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya Jumuiya ndogondogo za Afrika katika bara zima na kupata msaada mkubwa kutoka kila pembe. Kulingana nami, haya ni mafanikio makubwa zaidi. Kupitia mazungumzo haya, tutapata masuluhisho madhubuti ambayo yatashughulikia mianya iliyopo. Afrika itazungumza kwa sauti moja kwenye ajenda yetu ya bishara ndogondogo.

Twambie zaidi kuhusu Mkutano wa Mazungumzo kuhusu Mifumo ya Chakula

Unapoanza mazungumzo na una watu wengi wanaokusikiliza, wakichangia na kuunga mkono matendo yako yaliyopendekezwa na kukuamini, basi tayari unaleta mageuzi.

Ninajivunia juhudi zangu na wale wote ambao wanaamini juhudi zetu. Watu wamejitolea kwa majadiliano; wanashiriki na kutoa ushuhuda kuhusu tajriba zao halisi na wanatarajia masuluhisho ambayo yatasaidia biashara zao kupiga hatua. Wanajua tunazungumzia masuluhisho halisi na hivyo ni muhimu sana.