Kuwajulia hali wapendwa wangu kumekuwa muhimu sana

Get monthly
e-newsletter

Kuwajulia hali wapendwa wangu kumekuwa muhimu sana

-Dkt. Salah Okeel, Daktari wa Kimatibabu nyanjani nchini Misri
Africa Renewal
8 June 2020
Dr. Salah Okeel, Offshore Medical Doctor in Egypt
Dkt. Salah Okeel, Daktari wa Kimatibabu nyanjani nchini Misri

Tujulishe kidogo kukuhusu?

Jina langu ni Salah Okeel, nina umri wa miaka 36. Natoka El-Mahalla El-Kobra nchini Misri. Mimi ni daktari wa kimatibabu nyanjani wa Dharura na Huduma za kimatibabu nikifanya na shirika la Kimataifa la SOS.

Je, umekuwa ukifanya kazi kama mhudumu wa afya kwa muda gani? Je, nini ilikufanya kuchagua kazi ya huduma ya afya? Uko na hofu au majuto yoyote?

Imekuwa miaka saba ya kuridhisha kufanya kazi kama mhudumu wa afya. Kusaidia watu na kutoa huduma kwa wengine ni sehemu ya sababu ya kuchagua huduma ya afya kama taaluma yangu. Nafurahia kusema kwamba sina majuto yoyote katika kazi yangu, kujua kuwa mimi ni sehemu ya suluhisho ambayo inasaidia kuokoa maisha.

Je, unasaidiaje kupambana na COVID-19 katika nchi yako? Je, kazi yako imebadilikaje tangu kulipuka kwa COVID-19?

Huwa nahamasisha watu kila mara kuhusu COVID-19 katika eneo ninaloishi kwa sababu naamini inaweza kupunguza kuenea kwa virusi hivi. Pia hakujakuwa na mabadiliko makubwa kwa namna ninavyofanya kazi. Kuhakikisha usalama wa wagonjwa na wafanyakazi daima kumekuwa kipaumbele kwetu.

Je, nini inakuathiri sana katika janga hili la COVID-19? Je, nini inakufanya kuzidi kuendelea na unavyokabili hali hii?

Janga hili linaweza kulemea mtu na kuleta mfadhaiko. Nakuwa na mawazo kila wakati kuhusu jinsi ninavyoweza kuwasaidia kisaikolojia wafanyakazi wenza na kuwaweka salama dhidi ya COVID-19. Huku kukiwa na changamoto nyingi wakati huu mgumu, kuweka kituo cha kutenga watu tayari na kujitayarisha kumenisaidia kuondoa wasiwasi na kuweza kukabiliana vyema na hali hii.

Kwa mtazamo wako, ni mkakati gani, uliofanya vyema katika mapambano haya na nini haikufanya? Je, nini inafaa kufanywa kushinda vita dhidi ya COVID-19?

Kuwa na ufahamu, haswa kuhusu sasisho za hivi karibuni juu ya mlipuko huu, ni moja ya mikakati ambayo inafanya kazi vizuri katika eneo letu. Tunatekeleza hatua za uzuiaji na kuendelea kutoa ushauri kuhusu tahadhari za usalama kwa wafanyakazi wenza wote.

Je, ujumbe wako ni upi kwa watu wa nchi yako, na kwa wengine, wakati huu wa COVID-19?

Ujumbe wangu mkuu kwa Waafrika wenzangu ni kuchukua suala hili kwa uzito. Hakikisha wewe, na watu walio karibu nawe, munafuata hatua za uzuiaji wa COVID-19. Kuwajulia hali familia yako, marafiki na wafanyakazi wenzako wakati wa janga hili ni muhimu zaidi.