Wakazi wa Nairobi wahaha kujinasua wakati huu wa janga la virusi vya Corona

Get monthly
e-newsletter

Wakazi wa Nairobi wahaha kujinasua wakati huu wa janga la virusi vya Corona

UN News
29 May 2020
By: 
Grace akipita mbele ya duka lililofungwa akiwa anaelekea sokoni Kibera kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na Corona.
UNICEF
Grace akipita mbele ya duka lililofungwa akiwa anaelekea sokoni Kibera kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na Corona.

Wakati ulimwengu bado unaendelea kutafakari ni kwa zipi utashinda vita dhidi ya virusi vya COVID-19, mamilioni ya watu wamejikuta kwenye hali ambayo hawakutarajia. Baadhi ya nchi za Afrika bado zinaendelea kushuhudia kuongeza kwa maambukizi ya virusi vya Corona. Kwa mfano nchini Kenya idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa kasi suala ambalo limewatia hofu watu

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Covid-19 inapanda kwa kasi  hapa Kenya huku zaidi ya watu 1100 wakiwa tayari wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Pia zaidi ya watu 50 wameripotiwa kufariki kutokana na covid 19 hapa Kenya.

Hata hivvyo zaidi ya watu 380 waliogunduliwa kuwa na virusi hivyo awali kwa sasa wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa mujibu wa wizara ya afya.

Lakini kuna hofu kuwa huenda maambukizi zaidi yakashuhudiwa hapa Kenya hasa wakati huu inafanyika ya kuwapima watu zaidi anavyosema Dkt. Ahmed Khalebi ambaye ni Mkurugenzi wa maabara za Lancet zilizo na jukumu la kupima virusi hivyo.

Muda mfupi baada ya kisa cha kwanza kuthibitishwa Kenya, serikali ilichukua hatua za kuhakikisha kuwa virusi hivyo havienei jinsi ambavyo imeshuhudiwa katika zingine duniani.

Kwa mfano hoteli, shule, maeneo ya burudani, na hata makanisa yalifungwa na marufuku kwa mikusanyiko ya zaidi ya watu 50 zikatangazwa.

Lakini licha ya hofu iliyopo wengine wametaabika kuanzia wafanyubiashara hadi wanafunzi.Wizara ya afya imetahadharisha kwamba Kenya itashuhudia kiwango cha juu zaidi cha maambukizi ya virusi vya corona katika miezi ya Agosti na Septemba.

Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt Patrick Amoth amesema huenda Kenya ikaanza kuripoti visa 200 vya maambukizi ya virusi vya Corona kila siku.

Ametoa wito kwa wakenya kuendelea kuzingatia maagizo yaliyowekwa, akisisitiza kuwa idadi ya visa vya maambukizi itaendelea kupanda sambamba na ongezeko la idadi ya watu wanaopimwa.

Mnamo Machi 2020 Serikali ilibashiri kuwa huenda Kenya ingeandikisha angalau visa 10,000 vya maambukizi ifikapo mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Lakini sasa, Dkt Amoth anasema masharti ambayo serikali iliweka wakati huo, kama vile kufungwa kwa shule na kufungwa kwa Nairobi na Mombasa, yalipunguza kusambaa kwa virusi vya corona kwa kiwango kikubwa.