Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Ukuaji wa uchumi duniani watishiwa na COVID-19:UNCTAD

Get monthly
e-newsletter

Ukuaji wa uchumi duniani watishiwa na COVID-19:UNCTAD

UN News
10 March 2020
By: 
Masoko ya hisa duniani yamekuwa yakishuka thamani kadri mlipuko wa virusi vya corona unavyozidi.
UN Photo/Mark Garten
Masoko ya hisa duniani yamekuwa yakishuka thamani kadri mlipuko wa virusi vya corona unavyozidi.

Mgogoro wa kimataifa wa kiafya uliosababishwa na janga la virusi vya corona au COVID-19 unaweza kuwa na athari kubwa za kiuchumi, na kusababisha upungufu wa dola bilioni 2, 000, pamoja na dola bilioni 200 kwa nchi zinazoendelea, kulingana na moja ya matarajio mabaya yaliyotolewa leo Jumatatu kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD huko Geneva Uswis.

Kamati hiyo imesema kwamba "madeni, udanganyifu na kuteleza kwa kisiasa ni maeneo ambayo yanauwezekano wa kuleta athari za kiuchumi katika janga hili la kiafya.”

Kwa UNCTAT kusambaa kwa virusi vya Corona “Zaidi ya yote ni dharura ya afya ya umma lakini pia ni tishio muhimu la kiuchumi.”

Kamati hiyo imesema janga hilo la COVID-19 linaweza kusababisha mdororo wa kiuchumi katika baadhi ya nchi mwaka hu una kushusha kiwango cha kimataifa cha ukuaji wa kila mwaka kwa asilimia 2.5 kiwango kilichowekwa kimataifa cha ukuaji.

UNCTAD inasema sababu kubwa ni lupoteza imani kwa watumiaji na wawekezaji jambo ambalo ni ishara za haraka za kuenea kwa maambukizo, kulingana na utafiti.

Kwa mujibu wa mfumo wa awali, uchumi utakaoathirika zaidi utakuwa ni wa nchi zinazosafirisha mafuta, lakini pia wauzaji wengine wa malighafi. Wingine walio katika hatari ya mwisho kupoteza zaidi ya asilimia moja ya ukuaji uchumi ni , kama vile wale walio na uhusiano wa karibu wa kibiashara kwa chumi zilizoathirika hapo awali.

Katika suala hili, UNCTAD inakumbusha kwamba mzozo wa kifedha wa Asia wa mwishoni mwa miaka ya 1990 una kufanana na hali ya sasa. Isipokuwa tu kwamba mgogoro huo ulitokea kabla ya "Uchina kulipa eneo hilo jukumu kubwa zaidi la uchumi wa ulimwengu na wakati uchumi ulioendelea ulikuwa katika hali nzuri ya kiuchumi," imebaini UNCTAD, na kuongeza kuwa "hali hiyo si hali tena ya sasa"

COVID -19 kusababisha changamoto za kiuchumi kote duniani
COVID -19 kusababisha changamoto za kiuchumi kote duniani
MSC shipping

Kusuasua kwa uchumi kunatarajiwa Marekani

Kudorora kwa uchumi kwa kati ya asilimia 0.9 na 0.7 kunawezekana kutokea katika nchi kama Canada, Mexico na ukanda wa Amerika ya Kati. Hizi ni nchi ambazo zinajihusisha sana na mnyororo wa kimataifa wa thamani wan chi za Mashariki na Kusini mwa Asia nan chi zilizo katika uharaka Zaidi za Muungano wa Ulaya.

Tishio linguine linaloogopwa Zaidi na wataalam wa uchumi wa UNCTAD ni kwamba “katika nchi nyingi zinazoendelea kwa ujumla kiwango cha madeni ya umma nay a binafsi kimeshafikia pabaya”. Kuanzia Buenos Aires hadi Beirut na kuanzia Maputo hadi Islamabad, pia nchi zinzoendelea ambazo ziko katika makundoi tofauti ya kiuchumi na yanamfumo tofautitofauti wa kiuchumi wanakabiliwa na changamoto kubwa ya mzigo wa madeni.

Ripoti ya UNCTAD inasema karibu nusu ya nchi masikini kabisa zinazostahili kupata ufadhili kutoka kwa wakfu wa kupunguza umasikini na ukuaji wa uchumi au (PRG) zimefanyiwa tathimini na shirika la fedha duniani IMF na kubainika kwamba ziko katika hatari kubwa ya mzigo wa madeni ya nje au tayari zimezidiwa mna mzigo wa madeni ilipofika mwisho wa mwaka 2019.

Kwa mwaka 2018 jumla ya madeni katika nchi zinazoendelea yale ya binafsi, umma, ya ndani na ya nje yalifikia asilimia 191 ya jumla ya pato lao la ndani ikiwa ni kiwango kikubwa Zaidi kuwahi kurekodiwa Ikwa mujibu wa UNCTAD.

Kwa kuongezea, China imekuwa chanzo muhimu cha kukopa kwa muda mrefu kwa nchi zinazoendelea. "Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na mlolongo wa udhaifu wa kifedha na madeni ambayo yanazidi kuongezeka na ambayo hayaendani vyema na uwezo wao wa kuhimili mshtuko mwingine kutoka nje," amesema mkurugenzi wa idara ya utandawazi. kutoka UNCTAD, Richard Kozul-Wright, alipotoa mfano katika taarifa kwa waandishi wa habari.

Takwimu kutoka karibu nchi 117 zinazoendelea zinaonesha kuwa karibu moja ya tano ya uchumi huu una hatari sana kwa athari za moja kwa moja za mshtuko wa Covid-19 kutokana na mchanganyiko wa kudorora kwa mnepo wa madeni na ukubwa wa madeni yao, uchumi wa biashara na uhusiano mkubwa wa kiuchumi na Uchina. Nchi hizo ni pamoja na  Mongolia, Angola, Gabon, Ufilipino, Msumbiji, Vietnam, Kambodia na Zambia. Kulingana na shirika la UNCTAD, uchumi huu unaoendelea "unahusishwa kwa karibu na uchumi wa China" kupitia ushiriki wao katika minyororo ya thamani ya kimataifa inayoongozwa na Wachina na pia inategemea usafirishaji wa malighafi kwenda China.

Athari za uwezekano wa mgogoro wa madeni

Kwa kuongezea, Beijing imekuwa chanzo muhimu cha fedha kwa nchi zinazoendelea, na mikopo kwenda katika soko na uchumi unaoibuka wa mipakani ambao unaongezeka mara kumi (kutoka dola bilioni  $ 40, kwa 2008 hadi $  dola bilioni 400, kwa mwaka 2017).

Kwa nchi kama Zambia, Mongolia, Ecuador, Venezuela, Angola, Kenya, Pakistan, Sri Lanka, Bolivia na Jamaica, China sasa ndiyo mkopeshaji mkuu rasmi.

Katika hali hii UNCTAD inaamini kwamba ikiwa hali hizi za kukopesha zitaimarika na kukosekana, wale walio na uhusiano mkubwa wa kifedha na China wanaweza kuwa kati ya wale ambao watapata ugumu zaidi kupona kutokana na athari za kiuchumi za mlipuko wa Covid-19.

Kwa upana zaidi, kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa mchanganyiko wa upungufu wa bei ya mali, mahitaji ya chini ya jumla, kuongezeka kwa madeni na mgawanyiko mbaya wa kipato pia "vinaweza kusababisha mzunguuko mbaya zaidi.