Ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu-Antonio Guterres

Get monthly
e-newsletter

Ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu-Antonio Guterres

UN News
By: 
Vijana wa kike na wa kiume wanashiriki kwenye programu za kuelimisha umma kuhusu madhara ya ukeketaji na wito unaotolewa juu ya utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia. Warren Bright/UNFPA Tanzania
Warren Bright/UNFPA Tanzania. Vijana wa kike na wa kiume wanashiriki kwenye programu za kuelimisha umma kuhusu madhara ya ukeketaji na wito unaotolewa juu ya utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijana
Warren Bright/UNFPA Tanzania. Vijana wa kike na wa kiume wanashiriki kwenye programu za kuelimisha umma kuhusu madhara ya ukeketaji na wito unaotolewa juu ya utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.

Leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji, FGM, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake uliotolewa mjini New York Marekani amesema ukeketaji ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaochukiza na ambao unadhuru wanawake na wasichana kote duniani. Unawanyima utu wao, unahatarisha afya yao na kusababisha maumivu yasiyo na sababu, hata kifo.

“Ukeketaji umejikita katika kukosekana kwa usawa wa kijinsia na unaendeleza hayo kwa kuminya fursa kwa wasichana na wanawake kutambua haki na uwezo wao kamilifu. Takribani wanawake na wasichana milioni 200 walioko hai hii leo wameathiriwa na ukeketaji. Na kila mwaka takribani wanawake milioni 4 wako hatarini kukeketwa” ujumbe wa Katibu Mkuu Antonio Guterres umbainisha.  

Aidha ujumbe wa Guterres umeeleza kuwa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, yanatoa wito wa kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka 2030. Umoja wa Mataifa unaungana na juhudi za ulimwengu, kikanda na kitaifa katika kulifikia lengo hilo. Kukabiliana na ukeketaji ni sehemu kubwa ya jitihada zetu katika mpango uliozinduliwa kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya ili kukomesha aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.

Guterres ameongeza kusema kuwa kutokana na utashi wa kisiasa, tunaona mabadiliko chanya katika nchi kadhaa. Hata hivyo ikiwa mwelekeo wa sasa utaendelea, mafanikio yaliyopatikana yatazidiwa kasi na ongezeko la idadi ya watu kwenye maeneo ambako mila hii potofu inatekelezwa.

“Katika siku hii ya kutokomeza ukeketaji, ninatoa wito wa kuongeza hatua za kidunia za pamoja za kutokomeza ukeketaji wanawake na kuzingatia kwa dhati haki za binadamu za wanawake na wasichana.” Guterres amesisitiza.