Sauti ya juu inaua ngoma ya msikio kwa vijana muongozo watolewa:WHO

Get monthly
e-newsletter

Sauti ya juu inaua ngoma ya msikio kwa vijana muongozo watolewa:WHO

UN News
By: 
Mebratu almaarufu Tanki ni mvulana wa miaka 16 kutoka Eritrea. Muziki ni moja ya vitu anavyopenda, anapenda kusikiliza nyimbo za kitamaduni kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani. Picha: © UNICEF/UN0264259/Haro
Picha: © UNICEF/UN0264259/Haro. Mebratu almaarufu Tanki ni mvulana wa miaka 16 kutoka Eritrea. Muziki ni moja ya vitu anavyopenda, anapenda kusikiliza nyimbo za kitamaduni kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani.
Picha:© UNICEF/UN0264259/Haro. Mebratu almaarufu Tanki ni mvulana wa miaka 16 kutoka Eritrea. Muziki ni moja ya vitu anavyopenda, anapenda kusikiliza nyimbo za kitamaduni kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani.

Vijana zaidi ya bilioni moja wa umri wa kati ya miaka 12 na 35 wanajiweka katika hatari ya kupata uziwi usioweza kutibika kwa sababu ya kusikiliza sauti za juu za vitu kama muziki kwa kutumia simu za kisasa za rununu zinazoweza kufanya mambo mengi.

Onyo hilo limetolewa leo na wataalm wa shirika la afya ulimwenguni WHO, wakizindua muongozo mpya wa kusaidia kushughulikia tatizo hilo.

Mapendekezo yaliyotolewa na muongozo huo kupunguza tatizo la wengi kupata uziwi kwa kusikiliza sauti za juu ni pamoja na utendaji mzuri wa vifaa vya kusikilizia ambavyo vinaweza kudhibiti uwiano wa sauti ikiwa ni ya juu sana, muda ambao watu wanasikiliza muziki kutumia vifaa hivyo.

Mtaalam wa kiufundi wa WHO anayehusika na masuala ya kuzuia uziwi na kupoteza uwezo wa masikio kusikia katika shirika la WHO, Dkt. Shelly Chadha amesema “Vijana zaidi ya bilioni moja wako hatarini kupata uziwi kwa sababu tu ya kufanya kile wanachokifurahia zaidi mara kwa mara , ambacho ni kusikiliza muziki kupitia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani (headphones)”  ameongeza kuwa “kwa wakati huu hatuna kitu chochote kinachoshikika isipokuwa ni hisia zetu tu zikituambia ‘unachofanya ni sahihi, au je hiki ni kitu ambacho kitatusababishia kupoteza uwezo wetu wa kusikia au uziwi katika miaka michache ijayo?”

Mradi wa pamoja wa shirika la kazi duniani (WHO) na Muungano wa kimataifa wa mawasiliano (ITU), ni jaribio la kutaka kukabiliana na tatizo la kutokuwa na ufahamu kuhusu athari za kusikiliza kelel kubwa hwakati kukiwa na takwimu zionyeshazo kwamba, takriban asilimia 50 ya vijana wanasikiliza sauti katika viwango visivyo salama kupitia vifaa binafsi zikiwemo simu za kisasa za rununu ambazo matumizi yake yanaendelea kuongezeka duniani.

Kwa mujibu wa WHO leo hii tatizo la kupoteza uwezo wa kusikia ambalo halijashughulikiwa inaugharimu uchumi wa dunia dola milioni 750.

Mapendekezo

Dkt. Chadha amesema “inabidi kufikiria kwamba suala hili ni kama kuendesha gari kwenye barabara kuu lakini bila kuwa na kidhibiti mwendo. Na tulichokipendekeza ni kwamba simu za kisasa za rununu zije zimewekwa vifaa vya kudhibiti sauti ambavyo vyakuwa vinakuelezea ni kiwango gani cha sauti unakipata na kukujulisha endapo kimepindukia ama la.”

Chaguo la wazazi kudhibiti sauti pia lijumuishwe. Mapendekezo haya yamejumuishwa pia kwenye mapendekezo ya Umoja wa Mataifa kwa sekta husika  ambayo ilishiriki katika miaka miwili ya majadiliano  sambamba na wataalam kutoka serikalini, vyombo vinavyohusika na wanunuzi na asasi za kiraia.

Muongozo huu mpya pia unapendekeza kutumia teknolojia ili kuandaa wasifu wa wasilikilizaji kwa kufuatilia ni kwa kiasi gani wanatumia vipokea sauti vynavyobanwa kichwani, na kisha kuwajulisha ni kwa kiasi gani matumizi yao ni salama ama la. Na teknolojia hiyo amesema Dkt. Chadha “ni ile ya kudhibiti moja kwa moja au kupunguza sauti bila mtumiaji kufanya hivyo ili wakati ambapo mtumiaji anazidi kiwango cha sauti inayostahili kifaa hicho kinapunguza chenyewe ili asiathiri masikio yake.” Kwa mujibu wa WHO zaidi ya mtu mmoja kati ya 20  miongoni mwa watu wazima milioni 432 na watoto milioni 34 ana matatizo ya kupotea kwa uwezo wa kusiki au uziwi ambao unaathiri maisha yake.

Utafiti wa WHO umebaini kwamba waathirika wengi waanishi katika nchi masikini au za kipato cha wastani na kwamba ifikapo mwaka 2050 zaidi ya watu bilioni 900 watakuwa na matatizo ya uwezo wa masikio kusikia.Dkt. Tedros Gebreyasus ambaye ni mkurugenzi mkuu wa WHO anasema karibu nusu ya visa vyote hivyo vinaweza kuepukika kwa kuschukua hatua za afya ya jamii, akiyasema hayo kuelekea “siku ya kusikia duniani” ambayo kila mwaka hua Machi 3. Amesisitiza kwamba “ukizingatia ujuzi upo na teknolojia tunayo ya kuzuia uziwi soni ni kwa nini vijana waendelee kuharibu ngoma zao za masikio wakati wakisikiliza muziki. Ni lazima waelewe kwamba pindi watakapopata uziwi basi hawawezi kusikia tena.

Mada: