Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN

Get monthly
e-newsletter

Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN

UN News
By: 
Rose Luangisa mshiriki wa maonesho ya sanaa ya Umoja wa Mataifa yafahamikayo kama 'Sanaa kwa ajili ya amani' jijini New York Marekani. Picha: UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya
Picha: UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya. Rose Luangisa mshiriki wa maonesho ya sanaa ya Umoja wa Mataifa yafahamikayo kama 'Sanaa kwa ajili ya amani' jijini New York Marekani.
Picha: UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya. Rose Luangisa mshiriki wa maonesho ya sanaa ya Umoja wa Mataifa yafahamikayo kama 'Sanaa kwa ajili ya amani' jijini New York Marekani.

Mbali ya kuburudisha , kuelimisha na kuleta kipato kwa maelfu ya watu wanaoikumbatia, sanaa pia ni chachu ya kuchagiza amani kwakuwa inawaleta watu pamoja, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Sanaa ni moja ya mbinu zinazotumiwa na Umoja wa Mataifa kueneza amani na kuondoa migogoro kote duniani. Aidha Sanaa inatumika pia kama ajira. N amiongoni mwa wanaoitumia Sanaa kujipatia kipato ni Bi Rose Luangisa ambaye ni mtayarishaji wa maonesho ya vitu vya asili kutoka barani Afrika na mwaka huu wa 2019 ameshiriki katika maonesho ya Sanaa ya Umoja wa Mataifa yaliyopewa jina ‘Sanaa kwa ajili ya amani’ yakifanyika katika makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani. Baada ya maonesho hayo Bi Luangisa ameketi na UN News Kiswahili kuzungumzia suala hilo. Akizungumza nami ameanza kwa kuelezea watu wanavyofaidika na shughuli za Sanaa.