Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Mwalimu Tabichi ang'ara tuzo ya Umoja wa Mataifa

Mwalimu Tabichi ang'ara tuzo ya Umoja wa Mataifa

25 October 2019
UN Kenya/ Tirus Wainaina. Peter Tabichi, mshindi wa tuzo ya mtu wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya mwaka 2019 na mshindi wa tuzo ya mwalimu bora duniani 2019.
UN Kenya/ Tirus Wainaina. Peter Tabichi, mshindi wa tuzo ya mtu wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya mwaka 2019 na mshindi wa tuzo ya mwalimu bora duniani 2019.

Mwalimu Peter Tabichi ambaye amepata umaarufu mkubwa  baada ya kutunukiwa tuzo ya mwalimu bora duniani mwaka 2019 , sasa ameibuka kidedea tena na kuwa mshindi wa tuzo ya mtu bora kwa Umoja wa Mataifa nchini Kenya mwaka huu. Tuzo ambayo hutolewa nchini humo kwa mtu ambaye ameleta mabadiliko chanya katika jamii yake.

Akizungumza na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC jijini Nairobi Kenya pindi tu baada ya kupokea tuzo hiyo Alhamisi, Bwana Tabichi ameelezea maana ya tuzo hiyo kwake.

(Peter Tabichi)

Ama kweli mafanikio ya mtoto ni juhudi za mzazi  na baba yake mzazi Lawrence Tabichi  hakuficha furaha yake.

(Baba Tabichi)