Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Mtoto wa miaka 4 anajisiwa Somalia, UNFPA yazungumza

Get monthly
e-newsletter

Mtoto wa miaka 4 anajisiwa Somalia, UNFPA yazungumza

UN News
18 May 2020
By: 
Wasichana wakiwa katika kibanda cha walionyanyasiwa kijinsia Mogadishu. Baaadhi wanaweza kupata ajira katika duka mama mmoja mjini humo la vitambaa.
UNICEF/Holt
Wasichana wakiwa katika kibanda cha walionyanyasiwa kijinsia Mogadishu. Baaadhi wanaweza kupata ajira katika duka mama mmoja mjini humo la vitambaa.

Taarifa ya UNFAPA iliyotolewa leo mjini Mogadishu, Somalia, inasema kuwa mtoto huyo wa kike alifanyiwa kitendo hicho tarehe 14 mwezi huu wa Mei huko Madina mjini Mogadishu.

“Tunalaani vikali kitendo cha kunajisiwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 4. Tunalaani vikali ukatili huu wa kingono wa kutisha. Ni kwa masikitiko makubwa tunaendelea kushuhudia visa vya aina hii nchini Somalia,” imesema taarifa hiyo.

Shirika hilo limesema linasimama kwa mshikamano na familia ya mtoto huyo, “na tunatoa wito kwa mamlaka kuongeza kasi ya uchunguzi wa kisa hiki na tunatoa wito ufanyike mchakato sahihi wa kimahakama.”

Halikadhalika UNFPA imesisitiza wito wake wa kutaka kupitishwa na kuwa sheria kwa muswada wa sheria ya makosa ya ukatili wa kingono, muswada ambao imesema umesalia bungeni muda mrefu bila kupitishwa.

“UNFPA Somalia inatoa wito wa kuimarishwa kwa mifumo ya ulinzi wa wanawake na watoto ambao wameendelea kuwa hatarini kukumbwa na ukatili wa kijinsia,” imesema taarifa hiyo ikitamatisha kuwa leo na kila siku, “hebu na tutetee haki za binadamu, usalama na utu wa kila mwanamke na kila mtoto wa kike popote pale alipo.”