MONUSCO na harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini DRCMONUSCO na harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini DRC

Get monthly
e-newsletter

MONUSCO na harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini DRCMONUSCO na harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini DRC

UN News
1 April 2020
By: 
Walinda amani wa MONUSCO wameweka mikakati kudhibiti kuenea kwa COVID-19
MONUSCO/Michael Ali
Walinda amani wa MONUSCO wameweka mikakati kudhibiti kuenea kwa COVID-19

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ambao wamethibitishwa hadi leo hii ni 109 huku 8 (wanane) kati yao tayari wamefariki dunia, Umoja wa Mataifa umechukua hatua kuunga mkono hatua za serikali za kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi hivyo miongoni mwa wananchi wanaowahudumia na wafanyakazi wake.

Mathalani ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umechukua tahadhari hizo na baadhi ya hatua ni  kupunguza doria, kufuta safari zisizo za lazima ndani ya nchi, kufanya mikutano muhimu kwa kutumia teknolojia ya video ili kupunguza hatari zaidi.

Aidha timu ya matabibu kutoka MONUSCO imejiandaa na inafuatilia hali kwa karibu huku wakielezea kile wanachofanya kama anavyofafanua Sajini Ibrahim,  mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania.

"Tunanawa mikono kwa ajili ya kuweza kujikinga kutokana na Corona, lakini hatukuanza sasa ila wakati wa mlipuko wa ebola kwa hiyo kumekuwa na mwendelezo kwa ajili ya kuweza kujikinga na pia tunazingatia namna ya kusalimiana kwa kutumia miguu na kuwa mbali. Kwani kunawa mkono ndio msingi katika kujikinga kutokana na korona ukizingatia sehemu mbali mbali ambazo mikono inagusa."