Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Makala ya maoni: Ni sharti tuchukue hatua hivi sasa kuzuia tatizo la ukosefu wa chakula barani Afrika, asema Naibu Mkuu wa FAO

Get monthly
e-newsletter

Makala ya maoni: Ni sharti tuchukue hatua hivi sasa kuzuia tatizo la ukosefu wa chakula barani Afrika, asema Naibu Mkuu wa FAO

Afrika Upya: 
30 July 2020
By: 
Bi. Maria Helena Semedo
WHO
Bi. Maria Helena Semedo

Ushirikiano kati ya sekta kama vile kilimo, biashara, udhibiti wa majanga na ulinzi wa kijamii utakuwa muhimu mno katika ‘kujenga upya na vyema’ baada ya COVID-19

Janga la COVID-19 limewasili Afrika wakati bara hili tayari linakabiliwa na matatizo mengine. Bila shaka, kujengwa upya kwa Afrika baada ya janga hili kutakuwa shughuli kubwa ambayo itahitaji juhudi halisi, kutoka sekta kadhaa na zilizoshirikishwa pamoja.

Ukosefu wa chakula ulikuwa unatishia barani Afrika hata kabla ya kuibuka COVID-19. Zaidi ya Waafrika 256 milioni, au asilimia 20 ya idadi ya watu barani hawana chakula cha kutosha. Miongoni mwa hawa, milioni 73 wanakabiliwa na ukosefu mkuu wa chakula, na Afrika ina mataifa matano kati ya yaliyoratibiwa kama yanayokabiliwa na ukosefu wa chakula ulimwenguni.  

Matokeo ya lishe pia yanavunja moyo: Afrika ina watoto milioni 59 waliodumaa ilhali bara hili halitatimiza shabaha ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya kupunguza idadi ya watoto waliodumaa kwa asilimia 40 kufikia 2030.  

Hivi karibuni, mizozo iliwawacha watu milioni 33 katika mataifa kumi barani Afrika wakihitaji msaada wa dharura wa kibinadamu na ikawalazimisha wengine mamilioni kuhama makwao, na kuhatarisha utoshelevu wao wa chakula.

Wengine milioni 23 wanahitaji msaada kwa sababu ya matokeo ya tabianchi kama ukame, mafuriko na maporomoko ya ardhi. Hali ya hewa pia inajulikana kwa kuimarisha kuzaana kwa wadudu waharibifu kama Nzige wa Jangwani na Minyoo.

COVID-19 ni ongezeko kwa janga hili, inazidisha hali mbaya tayari ya ukosefu wa utoshelevu wa chakula, na kuwaathiri zaidi wanawake na wasichana ambao tayari wamo katika hatari.

Kuathiri mikondo ya thamani ya chakula kunaweza kusababisha bei za juu za chakula na uhaba, pamoja na uwezo wa kupata, chakula.

Wakulima wadogo, wafugaji wa kuhamahama na wakulima wafugaji wataathirika zaidi, kwa kuwa wana uwezo mdogo sana wa kuhimili athari za COVID-19, huku wakikabiliana na majanga mengine ya Nzige wa Jangwani, mafuriko na ukame mkuu.

Athari za kiuchumi za kipindi kifupi na kipindi kirefu za janga hili zitawasukumiza mamilioni zaidi katika tatizo la ukosefu wa utoshelevu wa chakula na utapiamlo. Katika hali yoyote ile, watakaoathiriwa zaidi ni maskini na wale walio katika hatari kuu katika jamii.

Lipi linastahili kufanywa?

Tatizo la COVID-19 limetambulisha wazi ukosefu wa usawa na hatari za watu fulani kukosa chakula, na hivyo hali ya kawaida haiwezi kuendelezwa. Kwa pamoja tuna nafasi ya kurekebisha na kugeuza mifumo ya chakula ili iwe nyumbufu na endelevu zaidi.

Lazima tuanze kupanga kuhusu ujenzi mpya na bora sasa ambao unaweza kusaidia kuongoza Afrika kwa njia salama, yenye afya na endelevu zaidi na ilio jumuishi. Sera zilizoshirikishwa vibaya zinahatarisha na kuzidisha ukosefu wa usawa usioendelevu, na kurejesha nyuma ufanisi uliopatikana katika kupunguza umaskini na kumaliza njaa.

Mshikamano ulioboreshwa kati ya sekta kama kilimo, biashara, kudhibiti majanga na ulinzi wa kijamii ni muhimu katika ‘kujenga upya vyema’.

Hakuna taifa wala shirika moja linaloweza kukabili maenezi ya COVID-19 na matatizo mengi peke yake. Juhudi za pamoja na kutoka kwa sekta mbalimbali zinahitajika kwa dharura ili kuepusha tatizo la ukosefu wa chakula barani Afrika, huku tukijianda kwa ujenzi mpya.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linakaribisha ahadi  ya hivi karibuni ya mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika kuwasaidia Waafrika walio hatarini zaidi kupata chakula na lishe; kuwapa Waafrika vizuizi vya kijamii; kupunguza vizuizi kwa usafiri salama wa watu muhimu, na kwa usafirishaji na uuzaji wa bidhaa na huduma; na kuiweka mipaka wazi kwa biashara ya chakula na kilimo katika bara hili. FAO linashirikiana na Umoja wa Afrika na wadau wengine kuyasaidia mataifa kutekeleza ahadi hizi.  

Shirika hili linasaidia wanachama kuendelea na mipango yao ya ulinzi wa kijamii – haswa kutuma pesa, mipango ya chakula kwa wanafunzi shuleni, na mipango ya kazi za umma. Mipango hii inakuwa na ufanisi inapopangwa na kutekelezwa vyema. Inapunguza umaskini na ukosefu wa utoshelevu wa chakula mbali na kuimarisha unyumbufu nyumbani, kujenga mtaji wa kibinadamu na kuharakisha shughuli za kilimo na zisizo za kilimo.

Aidha, linayahimiza mataifa kutekeleza sera za sekta ya afya ambazo zinawalinda wakulima wadogo kutokana na hatari za kiafya na gharama za juu za matibabu.

Huku likisaidia biashara ya kikanda na masoko ya nchini, ahirika la FAO linashughulikia namna mifumo ya chakula inavyostahili kugeuzwa ili iweze kuhimili hatari kama COVID-19 lakini pia kuongeza kasi ya hatua kuelekea kuafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.  

Kuyashinda matatizo ya sasa na kujenga unyumbufu ni mbinu za kuirejesaha Afrika katika njia ya maendeleo endelevu.

Tuchukue hatua sasa, upesi na kwa ujasiri, kabla matatizo mbalimbali hayajawaweka mamilioni ya watu katika hatari ya njaa na utapiamlo na kuwa vigumu kufikia maendeleo endelevu.

Afrika itashinda hatari hii, lakini ikiwa tu tunaweza kushirikiana, kwa umoja.

Mada: 
More from this author