Kukabiliana na moja wapo wa maadui wakubwa zaidi wa Afrika – Ukame

Get monthly
e-newsletter

Kukabiliana na moja wapo wa maadui wakubwa zaidi wa Afrika – Ukame

Afrika Upya: 
26 March 2021
Susan Ojochide commenced her PhD research in 2020 at Bayero University in Kano, Nigeria. She aims to develop a model integrating ground station meteorological data, earth observation data and climate models in northern Nigeria.
Susan Ojochide alianza utafiti wake wa PhD mnamo 2020 katika Chuo Kikuu cha Bayero huko Kano, Nigeria. Anakusudia kukuza modeli inayojumuisha data ya hali ya hewa ya kituo cha ardhi, data ya uchunguzi wa dunia na mifano ya hali ya hewa kaskazini mwa Nigeria.

Susana Ojochide (kutoka Nigeria) anazungumzia kuhusu utafiti wake ambao utachangia katika kukabiliana na moja wapo wa maadui wakubwa zaidi wa Afrika – ukame:

Tueleze kuhusu wewe. Ulizaliwa na kukulia wapi?

Nilizaliwa katika jimbo la Kwara, Magharibi mwa Nigeria na nikakulia jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria.

Ni kitu gani kilichokuhamasisha kuhusu sayansi kwa ujumla, hasa katika nyanja yako ya utafiti ?

Nilivutiwa na asili pamoja na mazingira tangu nilipokuwa na umri mdogo. Kwahivyo, daima nilijua kuwa nilitaka kusomea sayansi. Mabadiliko makubwa katika safari yangu ya kisayansi yalikuja wakati wa masomo yangu ya shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Kogi mjini Anyigba katikikati mwa Nigeria.  Niligundua kuwa pembezoni mwa mji kulikuwa na baridi zaidi kuliko katikati ambapo chuo kikuu kilikuwepo. Hali hii ilichochea hamu yangu zaidi ya kutaka kujua na kuelewa tofauti za nyuzijoto katika sehemu tofauti.

Kwa hiyo, kama sehemu ya masomo yangu ya shahada ya sayansi katika Jiografia na Mipango, nilifanya uchambuzi wa chuo hicho kama kisiwa chenye joto mjini. Niliendelea na masomo ya shahada ya uzamili (sayansi) katika chuo kikuu cha teknolojia cha Federal kilichoko Minna, jimbo la Niger kusoma tofauti za  nyuzijoto katika jimbo la Kano.

Utafiti wako unalenga nini katika shahada ya uzamifu?

Nilianza masomo yangu ya shahada ya uzamifu (PhD)  mwaka 2020, kwa udhamini wa Regional Scholarship and Innovation Fund (RSIF). Nimesajiliwa katika chuo kikuu cha Bayero Kano, Nigeria mwenyeji wa RSIF.

Utafiti wangu unatumia hifadhidata za uchunguzi wa ardhi na mifumo ya tabia ya nchi  kuchunguza ukame unaotokana na mabadiliko ya nyakati angani. Sehemu ninayoilenga ni kaskazini mwa Nigeria, eneo la nusu ukame  ambalo ni sehemu ya Sahel. Wakati mkoa huu ni mzalishaji mkuu wa nafaka nchini Nigeria, unakabiliwa na ukame wa kila wakati, na athari kubwa kwa usalama wa chakula.

Ninalenga kutengeneza mfumo unaounganisha taarifa ya hali ya hewa ya kituo cha ardhini, data za uangalizi wa ardhi na mifumo ya tabia ya nchi. Nitaendeleza sehemu ya masomo yangu kupitia programu ya miaka miwili katika taasisi ya rasilimali za asili-Natural Resources Institute (NRI), Chuo kikuu cha Greenwich Uingereza, kuchunguza mifumo ya tabia ya nchi kwa kutumia mifumo ya juu ya hesabu.

Utafiti wako unachangia vipi katika Malengo ya Maendeleo Endelevu?

Utafiti huu  unachangia hasa kwa maendeleao endelevu, lengo namba mbili: Kumaliza njaa. Ukame ni mojawapo wa vyanzo vikuu vya uhaba wa chakula nchini Nigeria.

Matokeo yangu yataongeza maarifa yaliyopo kuhusu jambo hili na pia kuchangia katika kuendeleza mifumo ya maonyo ya awali (early warning systems) ili kutabiri matukio ya uwezekano wa ukame. Matokeo yake yatawasaidia wataalam wa hali ya hewa na kilimo, wakulima, watoa maamuzi na wadau wengi katika uzalishaji wa kilimo.  Zaidi ya eneo la utafiti,  maarifa yanaweza pia kutumika kwa maeneo mengine yenye ukame barani kote.

Ni kina nani wamekuwa washauri wako wakuu  ?

Kwanza ni Profesa Salihu Danlami Musa, msimamizi wangu wakati wa masomo yangu ya shahada ya kwanza chuoni na mpenda mazingira ambaye alileta mbinu ya kuvutia ya kusoma kupitia mifano hai na uchambuzi ambao unaweza kutumika katika maisha halisi.

Pili ni Dkt. Michael Thiel aliyesimamia masomo yangu ya shahada ya uzamili na ambaye sehemu yake kuu ya utafiti ni kuhusu tabia nchi, matumizi ya ardhi, ufuniko wa ardhi na matumizi wa hisia kubaini sehemu katika kusomea mabadiliko ya tabia nchi Afrika. Amekuwa wa muhimu sana katika kukua kwangu, kunishauri katika hatua zote za utafiti na kunipa motisha katika safari yangu.

 

Mada: