Kitu gani kipo kwenye kabeji la Afrika? Mengi

Get monthly
e-newsletter

Kitu gani kipo kwenye kabeji la Afrika? Mengi

Sylvia Wairimu Maina (kutoka Kenya), anazungumza kuhusu utafiti wake wa shadada ya uzamivu (PHD) kuhusu lishe na faida za kiafya za kabeji la Afrika
Afrika Upya: 
26 March 2021
Sylvia Wairimu Maina, a PhD scholar at Sokoine University, Tanzania, conducting research at the Korea Institute of Science and Technology (KIST) in South Korea, where she is currently on sandwich placement. Her research aims to synthesize compounds in the
Sylvia Wairimu Maina (kutoka Kenya), anazungumza kuhusu utafiti wake wa shadada ya uzamivu (PHD) kuhusu lishe na faida za kiafya za kabeji la Afrika.
Sylvia Wairimu Maina, a PhD scholar at Sokoine University, Tanzania, conducting research at the Korea Institute of Science and Technology (KIST) in South Korea, where she is currently on sandwich placement. Her research aims to synthesize compounds in the
Sylvia Wairimu Maina

Tueleze kiasi kuhusu wewe. Ulizaliwa wapi na ulikulia wapi?

Nilizaliwa na kulelewa kijijini nchini Kenya. Nilisoma katika shule ya bweni, na nikajifunza kuwajibika na kujitegemea nikiwa na umri mdogo

Kitu gani kilichokuvutia kuhusu sayansi na hasa  eneo lako la utafiti.      

Hamasa  yangu katika bioteknolojia na afya, kwa kiasi kikubwa imechochewa na kumbukumbu za babu yangu ambaye alikuwa akitumia dawa kutokana na mimea ili kutibu kondoo  walioshukiwa kupata majeraha ya kuumwana nyoka.

Ulipata wapi shahada zako za awali?

Nina shahada ya kwanza ya Sayansi katika Biokemia na Baiolojia ya Masi (2011) na shahada ya pili ya Sayansi katika Biolojia ya Masi na Bioinformatics (2014), zote kutoka chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha  Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya.

African cabbage
Kabichi ya Kiafrika
Michael Hermann/http://www.cropsforthefuture.org/

Mshawishi wako mkuu ni nani?

Nimeshawishiwa na Daktari Florence Wambugu, mwanasayansi wa Kenya mashuhuri kwa kazi yake ya utafiti na mipango kuhusu uzalishaji wa ndizi kwa kutumia vikonyo kama njia ya kuimarisha usalama wa chakula barani Afrika.

Lengo lako la utafiti ni nini?

Utafiti wangu unakusudia kutambua na kuunganisha virutubisho vinavyopatikana katika kabichi la Kiafrika (kisayansi ikijulikana kama Cleome gynandra) ambavyo  vina thamani kwa afya ya binadamu na wanyama.

Ingawa kabeji hutumiwa sana kama mboga na mmea wa dawa, C. gynandra ni mojawapo ya mazao yaliyosahaulika barani Afrika – ambayo mara nyingi huwa na lishe bora na yanafaa zaidi kwa mifumo ya kilimo ya hapa Afrika kuliko mboga za kigeni.

Masomo yangu yanadhaminiwa na Mfuko unaojulikana kama Regional Scholarship and Innovation Fund (RSIF). Nimesajiliwa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Tanzania, na sasa niko katika mpango wa mabadilishano ya vyuo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Korea, Seoul, iliyoko Korea Kusini.

Umepiga hatua gani hadi sasa?

Nimefanya mapitio na kuchapisha taarifa kuhusu maarifa ya glososini, salfa inayopatikana kwenye mboga kama kabeji za Kiafrika, broccoli, brussel sprouts, sukuma wiki (kale) na mboga zinazotoka kwenye jamii ya kabichi.

Virutubisho hivi vina mchango muhimu katika afya ya binadamu na wanyama (tiba na kinga ya magonjwa), afya ya mimea (kemikali za ulinzi, biofumigants na biocides) na tasnia ya chakula (vihifadhi).

Utafiti huo pia unaonyesha sababu zinazoathiri asili na uwepo wa virutubisho vya kibailojia, ili kuongeza uelewa wa umuhimu wa kuvitumia ili kuboresha afya.

Utafiti wako unachangia nini katika  Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)?

Kwa upana, utafiti wangu unawiana na lengo namba mbili la Maendeleo Endelevu 2030: Kumaliza njaa. Kiini cha lengo hili ni uelewa kwamba mabadiliko makubwa ya mfumo wa chakula na kilimo ulimwenguni yanahitajikakama tunapaswa kuwalisha watu zaidi ya milioni 690 ulimwenguni ambao kwa sasa wana njaa.

Kutokana na hali ya kuwa na virutubisho vingi, mazao ambayo yamesahaulika barani afrika  ni njia muhimu ya kushughulikia utapiamlo, haswa njaa iliyofichika, barani Afrika.

Utafiti wangu utachangia maarifa ya kisayansi yanayohitajika sana, na vile vile mwamko wa kufungua uwezo kamili wa mazao haya yatima ya Kiafrika.

Safari yako ya masomo inachangia vipi kukabiliana na janga la COVID-19?

Nikiwa pamoja na wasomi wengine wawili wa kike wa RSIF PhD, nilihojiwa katika makala iliyozungumzia athari za janga la COVID-19 kwenye maisha yetu binafsi na safari za utafiti.

Tunaamini kuwa uwasilishaji dhahiri wa changamoto ambazo tumekabiliana nazo, mafunzo tuliyojifunza na vyanzo vyetu vya ushujaa vitasaidia kupunguza athari mbaya za janga hilo kwa wasomi na watafiti wengine.

 

Mada: