Ili tutimize SDGs Kenya lazima tuhakikishe huduma za afya kwa wote:Sicily Kariuki

Get monthly
e-newsletter

Ili tutimize SDGs Kenya lazima tuhakikishe huduma za afya kwa wote:Sicily Kariuki

UN News
25 September 2019
By: 
Waziri wa afya kutoka Kenya, Sicily Kariuki katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya
Waziri wa afya kutoka Kenya, Sicily Kariuki katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

Ili serikali ya Kenya ifanikishe utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s ifikapo mwaka 2030 ni lazima huduma za afya kwa wote zipatikane kuhakikisha nguvu kazi imara ya kusongesha mbele mchakato huo, amesema waziri wa afya wa nchi hiyo.

Akizungumza nami kandoni mwa mkutano ngazi ya juu UNGA 74, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani waziri Sicily Kariuki amesema Kenya inatambua umuhimu wa afya kwa wote na ndio maaana sasa iko katika mradi wa majaribio unaendeshwa kwapamoja na  shirika la afya duniani WHO. Waziri Kariuki amesema, "kama nchi tulianza mambo ya afya kwa wote Desemba mwaka uliyopita kwa ajili ya kuweka mkakati kuhakikisha afya wka wote kama Kenya tulisema tungetaka tujifunze ile ya nyumbani ili tukipata pengo tuweze kulitatua."

Je mradi huu umeanza na nani ? Waziri Kariuki amesema, "kaunti ambayo kuna maradhi ya kuambukizwa ambayo ni Kisumu alafu kaunti nyingine ilio na maradhi yasiyo ya kuambukizwa kama vile saratani, kisukari na magonjwa ya aina hiyo tukaneda Nyeri, tukachukua kaunti nyingine ambayo vifo vya mama na watoto viko juu ambayo ni Isiolo, hatimaye tukachukua kaunti ambayo ajalai za barabarani ziko juu ambayo ni Machakos."

 Ameongeza kuwa licha ya mafanikio ya kuwafikia takriban watu milioni 3 kwa huduma bure kabisaa kuna changamoto akisema, "Idadi ya watu ambao wanasaka huduma katika hospitali za serikali imeongezeka kwa asilimia 40 na zaidi kwa hiyo ni kumaanisha kama hatukuwa tumepata wahudumu wa kutosha na hvyo foleni hospitalini ni ndefu na hiyo si sawa ukizingatia aina ya matibabu unayokwenda kusaka kwa hiyo tunaona muhimu wa kusaka mafunzo na kuwawezesha wafanyakazi zaidi."

Waziri Kariuki amesema lengo ni kuwafikia Wakenya wote na wanatumia yale wanayojifunza katika mradi huo kuandaa mikakati thabiti.

Mada: