Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Hakuna kitabu alichoandika Profesa Waliaula kikapuuzwa – Mbotela

Get monthly
e-newsletter

Hakuna kitabu alichoandika Profesa Waliaula kikapuuzwa – Mbotela

UN News
20 April 2020
By: 
Je wazungumza Kiswahili?
UN News
Je wazungumza Kiswahili?

Kufuatia kifo cha aliyekuwa nguli wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya Profesa Ken Walibora Waliaula, baadhi ya watu waliomfahamu wametoa kauli zao juu ya mwendazake huyo ambaye pia alikuwa mwanahabari, mwandishi wa vitabu na mwanachama wa Chama cha Kiswahili cha kitaifa nchini Kenya, CHAKITA.

Dkt. Mwanahija Ali Juma.

Miongoni mwao ni Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili huko Zanzibar BAKIZA. "Profesa Ken Walibora ni Mtaalamu ni Mwandishi wa habari ni mwandishi wa vitabu ni Mwalimu lakini ni  mwanafastafa muhimu katika taaluma ya lugha ya kiswahili.Alikua tayari kuwakosoa baadhi ya watu kwa kuandika makala mbalimbali kwa kupitia magazeti na hasa gazeti la Taifa leo linalotoka kule  Kenya. Lakini pia alikua tayari kuandika kazi za fasihi katika njia tofauti. Kitabu chake kimoja chake ambacho ni maarufu sana ni  Siku Njema A good day  kimetafsiriwa kwa lugha ya kingereza na kifaransa ni riwaya nzuri ambayo inaelezea  mambo mengi na muhimu ya kimaisha .Jumuiya ya wanakiswahili ulimwenguni na duniani kote imehuzunika sana."

Onni Sigalla

Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA naye akafunguka, "Kikubwa zaidi ambacho Profesa Ken Walibora tunaweza tukamkumbuka ni pale ambapo alijaribu  kwa kushirikiana na wenzie kuandika Islahi mbalimbali katika programu ya Microsoft na Google za kiswahili. Mwafrika mashariki mwenzetu  ambaye alidhubutu na kujaribu kuingiza hizo isilahi za kompyuta katika mzuguko wa matumizi yake ya kawaida

Kwa hivyo Kifo cha Ken Walibora sio tu  kwamba kimeigusa familia mbali pia  kimewagusa familia ya waswahili wote waliofundishwa naye,Vyuo amabavyo amehudhuria  hata Marekani,Nchi mbalimbali,Kenya alikofanya kazi kama mwanahabari lakini pia amefanya kazi kubwa  ya kuandika vitabu ambavyo ameacha kama kumbukumbu katika ulimwengu huu wa lugha . Hivyo ni vitu ambavyo sitaweza kumsahau Profesa Ken Walibora."

Leonard Mambo Mbotela

Leonard Mambo Mbotela, mtangazaji nguli wa siku nyingi nchini Kenya, alikuwa rafiki wa karibu na mwendazake Ken ambapo akihojiwa na mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya, Jason Nyakundi, kuhusu kifo cha Ken, anasema,,"kusema ukweli ameacha pengo, bila kuongeza chumvi na masala, alikuwa na kipawa cha kuandika, manake hakuna kitabu hata kimoja ambacho aliandika kikadharauliwa."

Kuhusu kitabu ambacho Profesa Ken alikuwa anaandaa kuhusu Mambo Mbotela, Bwana Mbotela mwenyewe anasema kuwa, "alikuja kwangu ananiambia  Bwana Mambo wewe ni mtangazaji mashuhuri mwanahabari mashuhuri  waonaje kama tukija na kitabu kuhusu maisha yako? Nikamwambie Ken, hilo ni wazo nzuri sana niko tayari  endelea. Nilipomjibu naam,  hivyo tukapanga basi akaja hapa nyumbani kwangu Lang'ata akanihoji na kupiga picha na kadhalika .Akaniambia  sasa anaenda kuandika hicho kitabu . Kabla hajafa akanipigia simu na akaniambia naja  nyumbani turekebishe mawili matatu na kweli akaja hapa nyumbani tukakaa wiki tatu zilizopita tu  tukasikizliana na  akatoka akashika njia akaenda. Akaniambia usijali ntakupigia  tutapangapanga Mwezi wa Mei Mungu akipenda tutazindua kitabu. Hivyo ndivyo nilivyo kuwa na mpaka leo hii kitabu hicho alikiachia msaidizi wake ambaye amenipigia simu leo leo tu  akiniambia kwamba Ken ametuacha lakini kitabu kitaendelea na tutafanya uzinduzi mwezi huu wa tano."