Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar

Get monthly
e-newsletter

Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar

UN News
By: 
Dau la kijadi lenye urefu wa mita 9 lilolotengenezwa kwa tani 10 za mabaki ya plastiki, litakuwa dau la kwanza la aina yake kuzinduliwa na kuanza safari yake tarehe 24 mwezi huu wa Januari kutoka Lamu Kenya mpaka Zanzibar Tanzania. Picha: UN Environment
Picha: UN Environment. Dau la kijadi lenye urefu wa mita 9 lilolotengenezwa kwa tani 10 za mabaki ya plastiki, litakuwa dau la kwanza la aina yake kuzinduliwa na kuanza safari yake tarehe 24 mwezi huu wa Januari kutoka Lamu Kenya mpaka Zanzibar Tanzania
Picha: UN Environment. Dau la kijadi lenye urefu wa mita 9 lilolotengenezwa kwa tani 10 za mabaki ya plastiki, litakuwa dau la kwanza la aina yake kuzinduliwa na kuanza safari yake tarehe 24 mwezi huu wa Januari kutoka Lamu Kenya mpaka Zanzibar Tanzania.

Hatimaye dau la plastiki lililosafiri kilometa 500 kutoka Lamu, nchini Kenya hadi Mji Mkongwe, Zanzibar nchini Tanzania limetia nanga Unguja likiwa limetimiza azma yake ya  kuelimisha jamii zilipo pwani kwa Kenya na Tanzania kuhusu madhara ya plastiki kwa binadamu, mazingira na viumbe vya majini. 

Likiwa limebeba wanamazingira kutoka shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na kampuni iliyohusika na ujenzi, Flipflopi, dau hilo lilipata fursa kuhamasisha jamii hizo za pwani juu ya madhara ya plastiki.

Walikutana na wanafunzi, wanajamii na viongozi wa serikali na kubadilishana mawazo kuhusu jinsi ya kubadili mtazamo wa matumizi ya plastiki.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa baada ya dau hilo kutia nanga mji mkongwe, Mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini Tanzania, Clara Makenya amesema..

(Sauti ya Clara Makenya)

Na le lengo la safari limetimia

(Sauti ya Clara Makenya -2)

Dau hilo lililojengwa na Ali Skanda kwa tani elfu 10 za taka za plastiki lilianza safari yake tarehe 24 mwezi Januari huko Lamu, nchini Kenya na kupitia Kipini, Malindi,Watamu, Kilifi, Mombasa, Diani, Shimoni, Wete, Pemba Kusini, Nungwi na hatimaye  leo  tarehe 7 limetia nanga Mji Mkongwe Zanzibar.