Dau la plastiki ladhihirisha #BahariSalama yawezekana

Get monthly
e-newsletter

Dau la plastiki ladhihirisha #BahariSalama yawezekana

UN News
By: 
Mwanafunzi akifuatilia kwa makini na kuandika kwenye daftari lake wakati wa warsha huko Diani kandoni mwa ziara ya dau la Flipflopo lililotengenezwa kwa taka za plastiki. Picha: Flipflopi/FinneganFlint.
Picha: UN Environment. Dau la kijadi lenye urefu wa mita 9 lilolotengenezwa kwa tani 10 za mabaki ya plastiki, litakuwa dau la kwanza la aina yake kuzinduliwa na kuanza safari yake tarehe 24 mwezi huu wa Januari kutoka Lamu Kenya mpaka Zanzibar Tanzania.
Picha: Flipflopi/FinneganFlint. Mwanafunzi akifuatilia kwa makini na kuandika kwenye daftari lake wakati wa warsha huko Diani kandoni mwa ziara ya dau la Flipflopo lililotengenezwa kwa taka za plastiki.

Baada ya siku 14 za kupasua mawimbi kwenye bahari ya Hindi kutoka Kenya hadi Tanzania, hatimaye dau lililotengenezwa kwa taka za plastiki lilitia nanga Mji Mkongwe huko kisiwani  Unguja, Zanzibar Tanzania tarehe 7 mwezi Februari kwa mafanikio makubwa.

Safari hiyo ya kilometa 500 kwa lengo la kuchagiza bahari salama au #CleanSeas  na matumizi ya zaidi ya mara moja ya plastiki ilikuwa ni ya mafanikio kwa kuwa ilibadili mtazamo kuhusu matumizi ya plastiki miongoni mwa miji ambapo dau hilo lilitia nanga.

Tani 10 za taka za plastiki  zilizotumika kutengeneza Flipflopi yenye urefu wa mita 9 ni pamoja na kandambili chakavu ambazo ziliokotwa kwenye fukwe na miji ya Kenya na safari yake ilikuwa ni kichocheo kikubwa na simulizi dhahiri ya jinsi ya kukabiliana na changamoto kubwa inayokumba dunia hivi sasa; uchafuzi utokanao na taka za plastiki.

Safari ilianzia Lamu, na kupitia Kipini, Malindi,Watamu, Kilifi, Mombasa, Diani, Shimoni, Wete, Pemba Kusini, Nungwi hadi Mji Mkongwe Zanzibar.

Mwanzoni mwa safari mjini Lamu, Ben Morison ambaye ni mwanzilishi mwenza wa mradi wa Flipflopi akaweka bayana kuwa, “kumbuka safari hii si kwa ajili ya dau tu, tulitaka kuonyesha kuwa matumizi ya mara moja ya plastiki hayana maana yoyote. Tunatarajia watu duniani kote watahamasika na kusaka mbinu zao za kuchukua hatua na kutumia tena na tena plastiki ambazo wametumia.

Njiani warsha zilifanyika mfano za kupima kiwango cha taka ndogondogo kwenye maji ili wanafunzi na wananchi waelewe madhara ya taka za plastiki.

Mjini Mombasa hatua kubwa iliyofikiwa ni kufungwa kwa dampo la taka la Kibarani. Dampo hilo lilikuwa linachuruzisha taka zake za maji moja kwa moja baharini.

Goddfrey Nato  ambaye ni Waziri wa Mazingira kwenye Kaunti ya Mombasa alieleza kuwa “kuendelea kutumia eneo hilo la kutupa taka kulikuwa ni hatari kubwa kwa bayonuai ya bahari. Haikuwezekana tena kuendelea kulitumia kwa usalama wa mazingira.”

Hivi sasa taka zitatupwa kwenye eneo rafiki zaidi kwa mazingira.

Halikadhalika kukawepo na ahadi kutoka kampuni na taasisi 29 zikiwemo hoteli 17 zilizopo ufukweni Mombasa kupiga marufuku matumizi ya chupa na mirija ya plastiki na hoteli hizo ni pamoja na Tamarind na kundi la hoteli za Serena Inn .

UNEP nayo ilikuwepo Mombasa ambapo afisa wake kutoka ofisi ya Afrika, Cyrille-Lazare Siewe alisema wakati wa tukio hilo kuwa “kwa kuleta pamoja sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wote, hili ni jukumu la UN Environment sasa na tunatumai watu wengi zaidi wataungana nasi,na tunatumai nchi zote pia kote duniani zitachukua hatua na kusema tunataka kuleta mabadiliko, tunataka kupambana na uchafuzi wa mazingira.”

Safari ya kilometa 35 kutoka Mombasa hadi Diani ilitamatishwa na shamrashamra nyingi ikizingatiwa kuwa ni nyumbani kwa Dipesh, kiongozi wa mradi wa Flipflopi.

Msanii mashuhuri nchini Kenya Muthoni Ndonga ambaye ni balozi mwema wa mradi wa Flipflopi aliyeahidi kutumia kipaji chake kusaidia na kuchochea mapinduzi katika matumizi ya plastiki kwa kusambaza ujumbe ya kwamba matumizi ya mara moja tu ya plastiki hayana maana yoyote.

Akizungumza kwenye shamrashamra za kupokea dau hilo mjini Diani, Muthoni amesema, “tunaanza kubadili mazungumzo..tunapaswa kufikiria jinsi ya kutunga sheria na kuzisimamia kuhusu matumizi ya mara moja ya plastiki —lakini wakati huo huo kwa kuwa tayari tunazo plastiki lazima tufikirie jinsi gani tunaweza kuzitumia tena na tena kwa matumizi bora.”

Mabaharia wa Flipflopi wakiongozwa na nahonda Skanda wameonyesha matumaini makubwa kwani wao binafsi kupitia safari yao wameweza kuzungumza moja kwa moja na wananchi wapatao 1,000 na kuwajulisha umuhimu wa fikra mbadala katika kuondokana na taka za plastiki.