Uganda yafunga shule zote kuzuia hatari ya COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Uganda yafunga shule zote kuzuia hatari ya COVID-19

UN News
20 March 2020
By: 
Bustani ya amani katika shule ya Immaculate nchini Uganda ambayo ni sehemu ya programu ya UNESCO ya ASPnet
UNESCO
Bustani ya amani katika shule ya Immaculate nchini Uganda ambayo ni sehemu ya programu ya UNESCO ya ASPnet

Serikali ya Uganda imechukua hatua ya kufunga shule zote, masoko na mijumuiko yote ya umma kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19 kwenye nchi hiyo ambayo yenyewe hadi sasa haina mgonjwa hata mmoja lakini imezungukwa na nchi mlimothibitishwa mlipuko wa virusi hivyo. 

Hiyo ni sauti ya Rais Wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni akihutubia taifa kuhusu tishio la mlipuko wa virusi hatari vya COVID-19 akiwa kwenye ikulu ya Entebbe.

Ameamrisha taasisi za elimu zote ikiwemo vyuo vikuu kufunga kwa kipindi cha mwezi moja kuanzia Ijumaa ya tarehe 20 mwezi huu wa Machi 2020.

Pia amebana mikutano ya kisiasa na kijamii, kufungua maeneo ya ibaada, mahoteli, mabaa, klab za muziki,mabaa na masoko  yanayolema. Lakini tofauti na taasisi za elimu, agizo kuhusu mijumuiko hiyo limeanza kutekelezwa mara baada ya hotuba yake.

Raisi Museveni amesema hatua ya kufunga shule inalenga kuhakikisha kwamba wanafunzi wanarejea majumbani kwao kabla ya kisa chochote kuripotiwa ili kuepuka gharama na changamoto za kutafuta wanaoshukiwa kuambukizwa ikiwa kisa kitapatikana na kuwatawanya.

Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa.
Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.

Kuhusu usafiri wa ndege, hamna ndege kutoka Uganda itakata tena mawingu kuelekea katika nchi ambako virusi vya COVID-19 vimesambaa sana ikiwemo Ufaransa, Italia, Japan, Spain, Korea Kusini na China.

Amesema Waganda wote wanaorejea nyumbani kutoka nje watawekwa karantini ya lazima kwa siku 14 pindi wanapowasili kwenye uwanjawa ndege.

Uganda inapakana na Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tanzania, Kenya na Sudan Kusini ambazo zote tayari zimethibitisha visa vya COVID-19 isipokuwa Sudan Kusini kwa wakati taarifa hii iliandaliwa.

Hivyo Rais Museveni amewahimiza waanichi kuzingatia maelekezo ya wizara ya afya na shrika na afya ulimwenguni (WHIO).

 Amesisitiza suala la usafi na kushirikiana na wahudumu wa afya kuripoti kisa chochote kinachoshukiwa kuwa ni chaCOVID-19 mapema iwezekanavyo.