Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Baadhi ya watu hunyimwa hazi yao ya kumili ardhi: Ibara17 UDHR70

Baadhi ya watu hunyimwa hazi yao ya kumili ardhi: Ibara17 UDHR70

Wanawake kama hawa hunyimwa haki zao za kumiliki mali. Picha: UN Women Cape Verde
Picha: UN Women Cape Verde. Wanawake kama hawa hunyimwa haki zao za kumiliki mali.

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa  mwaka huu wa 2018 linatimiza miaka 70. Tamko hilo lina ibara 30 na leo inamulikwa ibara ya 17 inayozungumzia haki ya mtu kumiliki mali yeye mwenyewe au kwa ushirika na mtu mwingine au wengine.

Ibara hii inazingatia ukweli kwamba baadhi ya watu wananyimwa haki hiyo kwa misingi mbalimbali ikiwemo rangi, jinsia, kabila, dini au umri.

Ibara hiyo pia mtu asinyangangwe mali yake bila sheria.

Miongoni mwa mali zinazotajwa ni pamoja na kiwanja au ardhi ikimaanisha kuwa mtu yeyote ana haki ya kumiliki ardhi, ali mradi azingatie sheria. Hata hivyo katika jamii nyingi ikiwemo barani Afrika, umiliki wa ardhi umekuwa na changamoto kubwa hususan kwa wanawake na wasichana. Mfano tu ni nchini Ethiopia ambako ilikuwa ni shida ambapo raia wengi wa kawaida walipoteza mali hususan viwanja  kutokana na  kutokuwa na ushahidi.

Mfano ikiwa wanamiliki viwanja lakini hawana hati ya umiliki ndipo  serikali ikafanya mikakati ya  kuwaondolea adha hiyo kwa kuwapatia hati. Mmoja wa wa wanufaika ni mkulima  Melkam Amogne aliyepambana mpaka alipopatiwa  hati ya umiliki ndipo akapumua,“Na sasa ikiwa mtu yeyote atajaribu kunyanganya ardhi yangu na weza kumshataki”.

 Hilo ni moja wa dhirisho la ibara hiyo ya 17 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Jamii zingine huwa zinawabagua watu wa jinsia ya Kike hususan ikiwa wanawake wamepewa talaka au wamesalia wajane. Familia za wanaume hufanya kila juhudi kuwanyang’aya ardhi hiyo licha ya mwanamke huyo kuwa na watoto. Ethiopia pia ndiyo itakuwa mfano mwingine.

Katika kutilia mkazo ibara ya 17 ya tamko la haki za binadamu, pia sehemu nyingine ya ibara hiyo inasema kuwa Mtu asinyanganywe mali yake  bila sheria. Lakini mama mmoja wa watoto watano mwenye umri wa miaka miaka 45 yalimfika mazito. Mmoja wa watoto wake, Mengaw Simachew anaeleza magumu mama yake  aliyopitia kuweza kupata uhakika wa kumiliki mali yake yaani kipande cha ardhi,“Kabla ya hati ya kumiliki kutolewa kulikuwa na mivutano ya mipaka ya ardhi hiyo na watu wakiwa wanachukua  kwa nguvu ardhi ambayo haikuwa yao.”

Naye mjane Nitsu Simachew anasema anafurahi kupata hati inayoonyesha kama ndiye mmilikaji halali wa kipande hicho cha ardhi hivyo haki hutendeka kwenda na ibara ya 17 inayosema kuwa kila mtu ana haki ya kumiliki mali.

Mada: