Asante walinda amani wanawake kwa kutujali -Wanawake Beni, DRC

Get monthly
e-newsletter

Asante walinda amani wanawake kwa kutujali -Wanawake Beni, DRC

UN News
2 June 2020
By: 
Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wakizungumza na wanawake huko Beni, DRC.
TANZBATT 7/ Ibrahim Mayambua
Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wakizungumza na wanawake huko Beni, DRC.

Wanawake wa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,ameomba walinda amani wanawake kutoka Tanzania waendelee kuwaunga mkono kiuchumi na kijamii.

Katika maadhimisho ya siku ya walinda amani duniani hii leo, maudhui yakilenga wanawake walinda amani ni ufunguo wa amani ya kudumu, baadhi ya wanawake wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wameomba walinda amani wanawake kutoka Tanzania waendelee kuwaunga mkono kiuchumi na kijamii.

Mmoja wa wanawake hao ni Kassoki Vaytsora Nadine, Chifu wa Kata ya Matembo mjini Beni ambaye msingi wa maombi yake ni changamoto wanazozipata akizitaja kuwa ni:

Ya kwanza tunabakwa sana mwanamke tunabakwa sana sana hatujui kwa nini  hilo linakuwa tatizo la kwanza la pili ni mauji watoto wamebaki yatima wanateseka sana,akina mama hawapo na hata wanaume wameuwawa. Wanawake ni wengi sana,tumeshindwa kulea watoto hata kufanya shughuli zingine za maisha tunashindwa .Yametusumbua vichwa sana,sijui twende wapi ama turudi wapi  Wadada ombi kwenu tunawaomba msitusahau sana jinsi 

Lakini hajasahau fadhila kutoka kwa walinda amani wanawake kutoka Tanzania.

Lakini kuna siku walitukumbuka siku kuu  ya akina mama,walikuja wakafurahi na sisi hiyo ni shukrani kubwa sana kwetu

Nduvia Msenji, ambaye naye ni mkazi wa Beni Mavivi akafunguka..

Ya kwanza nilishukuru sana wakati tulienda kupika chakula ambacho walituletea tulishukuru sana na tukasema kumbe akina mama wanatukumbukaga tunawashukuru ,tulipika chakula,watu walikula na kushukuru sana. Hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza. Nimesema kumbe akina mama wanatukumbuka,nikasema mungu awazidishie na wasisahau na hii siku isikuwe ya kwanza waendelee vile .Na nyingine ya pili,tuko hapa mavivi hapa matembo hatuna tena nguvu ya kwenda mashamba kwenda kwa shamba kunataka nguvu....Mume wangu alienda shambani askari akamkuta huko na hii simu ndio ilifanya mume wangu kakufa. Na kukiwa na kitu kama hiki lazima na nikasema basi mungu ushukuriwe .Tunaogopa hata kukaa kwa nyumba kifo kitakukuta hata kwenye mlango. Wanawake waliokule wanakuja tunashirikiana hata siku moja na wao magumu ni mengi .Kula inakuwa ngumu,kusomesha watoto pia inakuwa ngumu

Na ombi lake sasa 

Naomba hata mkatukazanie kazi hata kama ni ya kulima yoyote ambayo itafaa,tunateseka sana tunataka amani basi mtusaidie ,wa mama maafisa watusaidie sana Wadada ombi kwenu tunawaomba msitusahau,jinsi wanaishi kule ndani wasitusahau sisi wamama sisi wanawake wenzao