Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Asante UNHCR huduma ya kangaroo imeokoa watoto wetu -Wakimbizi

Get monthly
e-newsletter

Asante UNHCR huduma ya kangaroo imeokoa watoto wetu -Wakimbizi

UN News
29 April 2020
By: 
Mtoto wa siku tisa wa kiume na mamaye kijijini Bambaya wilaya ya Fiama Chiefdom,Kono Nchini Sierra Leone
UNICEF/Phelps
Mtoto wa siku tisa wa kiume na mamaye kijijini Bambaya wilaya ya Fiama Chiefdom,Kono Nchini Sierra Leone

 Huduma ya rahisi lakini muhimu ya kangaroo ambayo inatolewa kwenye kambi ya wakimbizi ya Gado nchini Cameroon imekuwa mkombozi wa wa Maisha ya watoto wanaozaliwa njiti kambini hapo. 

Huduma ya rahisi lakini muhimu ya kangaroo ambayo inatolewa kwenye kambi ya wakimbizi ya Gado nchini Cameroon imekuwa mkombozi wa wa Maisha ya watoto wanaozaliwa njiti kambini hapo. 

Katika kituo cha afya kambini Gado wanawake waliojifungua watoto nyiti wako katika mafunzo maalum ya kuwalea watoto hao waliozaliwa kabla ya wakati kwa kupitia huduma ya kangaroo, ambayo ni ya kumbeba mtoto kifuani kutwa kucha ili kuhakikisha jito lake la mwili linakuwa la kawaida kupitia joto la mwili wa mama yake.

Mkimbizi kutoa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Amadou ndio kwanza amejifungua mtoto wa kike njiti wa kike njiti, wanaye wawili wa kwanza walikuwa njiti pia na kwa bahati mbaya hawakuishi

Nilijifungua usiku alikuwa na uzito wa chini ya kilo mbili, alikuwa njiti kwani alizaliwa miezi miwili kabla ya wakati”

Kambi ya Gado inahifadhi wakimbizi zaidi ya 25,000 kutoka CAR na hospitali ndogo iliyopo haina huduma zote mfano umeme hukatika mara kwa mara na hakuna jenereta na pia haina vifaa vya kuhudumia watoto njiti, sasa wauguzi hawana jinsi bali ni kutumia mbinu ya asili ya kangaroo kwa wazazi kama Amadou

“Mkunga alinionyesha jinsi ya kutumia njia ya kangaroo na kumlinda mwanangu.”

Kabla ya huduma hii kambini hapa wanawake wenye watoto njiti walilazimika kujaza maji ya moto kwenye chupa za plastiki na kuviviringisha kwenye blanketi za watoto wao njiti ili kuwapa joto na ilikuwa hatari na wengi walipoteza Maisha.

Mwaka 2018 kupitia msaada wa shirika la wakimbizi UNHCR kwa ufadhili wa Bill na Melinda Gates wahudumu wa afya walipewa mafunzo ya huduma ya kangaroo ambayo sasa wanayotoa kwa wanawake wanaojifungua Watoto njiti kambini hapa. Miongoni mwa hudumu hao ni mkubga Monique Meka

“Tulikuwat unapoteza sana watoto kutokana na baridi, lakini asante kwa huduma hii licha ya tatizo la kukatika umeme  sasa tunaweza kuwalinda watoto katika joto linalotakiwa.”

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO kila mwaka huzaliwa watoto njiti zaidi ya milioni 20 dunini na zaidi ya asilimi 96 kati yao ni katika nchi zinazoendelea.