Usugu wa dawa za VVU waongezeka

Get monthly
e-newsletter

Usugu wa dawa za VVU waongezeka

WHO yatoa ripoti kuhusu usugu wa dawa za VVU 2021
World Health Organization
1 December 2021
Na: 

Ripoti ya Usugu wa Dawa za VVU ya WHO inatoa taswira ya kina kuhusu kiwango cha ukuaji wa usugu wa dawa, na hatua zinazochukuliwa na mataifa kuhakikisha watu watazipata dawa fanifu kutibu na kukinga VVU

Ripoti hiyo inafichua kwamba mwaka 2020, 64% ya mataifa lengwa (mataifa yenye mzigo mkubwa wa maambukizi ya VVU) yalikuwa na mipango tekelezi ya kitaifa kukinga, kuchunguza na kuwajibikia usugu wa dawa za VVU.

Mipango hii inaelekezwa na Mpango wa Kiutekelezi wa Ulimwengu kuhusu Usugu wa dawa za VVU 2017–2021, mpango wa washikadau wengi ulioshirikishwa na kuchapishwa na WHO.

WHO inayahimiza mataifa kuchunguza usugu na inapendekeza hilo kwa watu wanaoanza dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) iitwayo matibabu awali ya usugu wa dawa za VVU (PDR). WHO inapendekeza kwamba  wakati PDR kizuizi cha VVU-1 (NNRTI) kama vile nevirapine  na efavirenz kinapofikia kiwango wastani cha 10% kwa taifa linalochunguzwa, basi matibabu ya daraja ya kwanza ya VVU yanastahili kubadilishwa kwa dharura.

Ripoti hii inaonyesha kwamba mataifa zaidi yanafikia wastani huo wa 10% wa PDR wa usugu wa dawa za VVU kwa NNRTI na watu waliowahi kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU wanaweza kudhihirisha usugu wa dawa za daraja ya NNRTI mara tatu zaidi.

Matokeo haya yanasititiza haja ya kuongeza kasi ya mabadiliko ya utaratibu wa dawa za dolutegravir katika mataifa yanayoendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi za NNRTI.

Kwa kuzingatia matokeo ya hivi karibuni ya uchunguzi uliofanywa katika mataifa 10 ya Afrika Kusini mwa Sahara, zaidi ya nusu ya watoto wachanga waliogunduliwa na VVU wana VVU sugu kwa dawa kabla ya kuanza matibabu.  Matokeo haya yanaonyesha haja ya kuongeza kasi ya mabadiliko yanayoendelea na umuhimu wa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi za dolutegravir miongoni mwa watoto mapema iwezekanavyo.

Ukweli
  • Kufikia mwisho wa 2020, watu milioni 27.5 ulimwenguni walikuwa wakipokea matibabu ya kupunguza makali ya virusi. Usugu wa dawa za VVU unaweza kukwaza ufanisi wa dawa kupunguza makali ya virusi katika kupunguza visa vya VVU pamoja na uuguaji na vifo vinavyohusiana na VVU.
  • Kupunguza mweneo wa  usugu wa dawa za VVU ni kipengele muhimu  cha uwajibikiaji mpana wa kimataifa wa usugu wa dawa za kuua viini unaohitaji hatua zilizoshirikishwa katika sekta za kiserikali na ngazi za kijamii.
  • Katika chunguzi 21 kati ya 30 zilizoripotiwa kwa WHO, usugu wa dawa za VVU kabla-ya matibabu kwa  nevirapine (NVP) au efavirenz (EFV) miongoni mwa watu wanaoanza daraja ya kwanza ya ART ulifikia viwango vya 10%.
  • Usugu wa dawa za VVU kabla-ya matibabu kwa dawa ya daraja NNRTI ni kawaida mara tatu zaidi kwa watu waliowahi kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi.
  • Zaidi ya nusu ya watoto wachanga waliozaliwa na kina mama walioambukizwa VVU wana usugu wa dawa za VVU kwa moja au zaidi ya NNRTI.
  • Mweneo duniani wa usugu kwa dawa za daraja ya NNRTI unasisitiza haja ya kuongeza kasi ya mabadiliko katika utaratibu mpya wa dawa za dolutegravir.
  • Kusitisha usugu wa dawa za VVU ni muhimu katika kuhakikisha ufanifu wa kudumu wa uwepo wa dawa za kutibu VVU.
  • Kusitisha usugu wa dawa za VVU washikadau wote ulimwenguni wanastahili kuendeleza uwepo wa dawa bora za kutibu maambukizi ya VVU, kusaidia kusalia katika uangalizi na kutilia maanani matibabu, kuongeza upatikanaji na matumizi, upimaji wa idadi ya virusi ili kujua kama tiba ya VVU inafanya , na kubadilisha taratibu za matibabu kwa kasi tiba zinapothibtishwa kufeli.

Ripoti ya Usugu wa Dawa za VVU 2021

Siku ya Ukimwi Ulimwenguni 2021: Ujumbe kutoka Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Winnie Byanyima

Mpango wa Ulimwengu wa VVU  - Usugu wa dawa za VVU

Tangu 2019, WHO imependekeza matumizi ya dolutegravir kama dawa inayopendelewa ya daraja ya kwanza na ya pili kwa makundi yote ya watu. Ni bora zaidi, rahisi kumeza, na ina madhara mengine machache zaidi kuliko dawa nyinginezo zinazotumiwa sasa.

Dolutegravir pia ina kizuizi cha juu cha kijeni kukuza usugu wa dawa, na kwa hivyo kuwezesha kudumu kwake kwa muda mrefu na kwa ufanisi.

Tangu chunguzi hizo zilipotekelezwa, mataifa mengi zaidi yameanzisha mabadiliko hadi kwa utaratibu wa dawa za dolutegravir, kuwapa watu chaguo bora la matibabu na kuimarisha vita dhidi ya usugu wa dawa.  

Kinga ya kabla-ya-maambukizi  maarufu Pre-exposure prophylaxis (PrEP)  ndio chaguo fanifu la kinga kwa watu wasio na VVU ila walio katika hatari kuu ya kuambukizwa kama sehemu ya mielekeo jumuishi ya kinga. Usugu hutokea sana PrEP inapoanzia katika kuweka maambukizi hatari ya VVU ambayo hayajatambuliwa.

Huku mataifa yakitekeleza PrEP kukinga maambukizi ya VVU, kunastahili kuandamana na uchunguzi wa usugu wa dawa za VVU miongoni mwa watu wanaoambukizwa licha ya kutumia PrEP.

Ripoti hiyo inadhihirisha ya kwamba idadi ya mataifa yanayotimiza viwango vya juu vya ukandamizwaji wa virusi (≥90%) iliongezeka kutoka 33% mwaka 2017 hadi 80% mwaka 2020. Kutimiza viwango vya juu vya ukandamizwaji virusi miongoni mwa watu wanaopata matibabu ya kupunguza makali ya virusi kunakinga maambukizi ya VVU, kuugua na vifo vinvyohusiana na VVU na kuzuia kuibuka kwa usugu wa dawa za VVU.

Kuchunguzi idadi ya Virusi

Ripoti hiyo inasisitiza haja ya kuchunguza idadi ya virusi kila mara na kuwafuatilia watu wasiokandamiza virusi kwa karibu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha utaratibu wa matibabu wakibainishwa, ili kutimiza matokeo nafuu na endelevu kwa muda mrefu ya matibabu.

Aidha, kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa dawa bora za kutibu maambukizi ya VVU ni muhimu kuzuia usugu wa dawa za VVU.  

Matokeo haya yanasisitiza haja ya kuyasaidia mataifa katika kupata masuluhisho endelevu yaliyo faafu kwa miktadha ya jamii na yanaweza kujumuisha washiriki wa jamii au makundi ya uraia.

Huku  Mpango Tekelezi wa Ulimwengu kuhusu Usugu wa Dawa za VVU 2017–2021 unapokaribia, ripoti hiyo inapendekeza juhudi za siku za usoni za ulimwengu na kitaifa kutambua fursa zilizopo kuzuia, kuchunguza na kuwajibikia usugu wa dawa za VVU ikiwa ni pamoja na kujirekebisha kwa mazingira yanayobadilika kwa kasi ya matibabu na mifumo mipya ya kutoa huduma.

Kupunguza kuenea kwa usugu wa dawa za VVU ni kipengele muhimu cha uwajibikiaji mpana wa kimataifa kwa usugu wa dawa za kuangamiza viini unaohitaji hatua zilizoshirikishwa katika sekta zote za serikali na ngazi zote za jamii.

"Ripoti hii ya HIVDR abayo ni ya kawaida sasa na uchunguzi zinayajukuisha mataifa – kutoa matibabu ya ubora wa juu na uangalizi wa VVU na uwekezaji mahususi katika AMR. Katika siku za usoni, tutapanua uchunguzi wetu kwa ARV, zile zinazowasilishwa kama mawakala wa kudumu kwa kinga na matibabu – ili kudumisha ARV kwa watu wanaoishi na VVU," alisema Meg Doherty, Mkurugenzi wa Mipango ya Kimataifa ya VVU, Homa ya Manjano na Magonjwa ya zinaa.

Mada: