Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Kupodikasti kwapata umaarufu Afrika

Get monthly
e-newsletter

Kupodikasti kwapata umaarufu Afrika

Namna jukwaa la Afrika linavyozileta pamoja sauti katika chombo cha kijamii chenye msisimuo
Afrika Upya: 
6 May 2021
Mkurugenzi mwenza wa Africa Podfest Melissa Mbugua anaandaa tamasha hilo moja kwa moja kutoka Baraza
Marcus Olang
Mkurugenzi mwenza wa Africa Podfest Melissa Mbugua anaandaa tamasha hilo moja kwa moja kutoka 'Baraza Media Lab' Nairobi, Kenya

Josephine Karianjahi ni mshauri wa kimataifa kuhusu maendeleo mwanapodikasti kutoka Nairobi, Kenya. Kama Mkurugenzi mwenza wa Africa Podfest na mwenyeji wa podikasti ya ‘This I Can Do’, Bi. Karianjahi huwezesha mabadiliko ya kijamii kupitia kwa ushirikiano na ujumuishwaji katika upodikasti. Katika Makala hii, anaelezea malengo ya Africa Podfest na changamoto zinazowakabili wanapodikasti wa Afrika:

Wazo la Africa Podfest, ukumbi wa kijamii, lilitokana na tajriba yangu ya kupodikasti na ya mwasisi mwenza wangu katika kipindi ambapo sauti za Kiafrika zilikuwa karibu nadra kupata katika ulingo wa kimataifa wa kupodikasti.  

Africa Podfest ni kampuni inayoongozwa na wanawake na iliyoko Kenya, inayostawisha mazingira ya sauti ya Afrika. Huku likiwalenga wanapodikasti wa Afrika, jukwaa letu linafanya kazi kwa jumla kuinua utajiri wa uanuwai wa hadithi za Afrika ambazo hazijawa za kawaida katika vyombo vya kawaida vya   habari

Tunajibidiisha kuwawezesha wanapodikasti wote na ambao kama watu wachanga, watu walio na ulemavu, wanawake, watu wasio na pesa na juuiya ya mashoga wamekikumbatia chombo hiki kama watunzi maudhui na wasikilizaji.

Podikasti zilizokuwa barani Afrika zimekuwepo kwa kipindi kisichozidi mwongo mmoja. Tangu mwasisi mwenza Melissa Mbugua alipoanza kufuatilia ukuaji wake mwaka 2018, idadi yazo imeendelea kukua hatua kwa hatua kati ya 2017 na 2021.  

Africa Podfest co-director Josephine Karianjahi co-hosts the festival live from Düsseldorf, Germany.
Mkurugenzi mwenza wa Africa Podfest Josephine Karianjahi ndiye mwendeshaji wa sherehe hiyo moja kwa moja kutoka Düsseldorf, Ujerumani.

Wanapodikasti wanaweza kupatikana kokote katika bara hili– kuanzia Misri hadi Afrika Kusini, Nijeria hadi Kenya.  Hifadhidata yetu ya African Podcast inayotokana na umati imekuwa ikifanya kazi kuanzia 2019 na idadi ya podikasti ziwasilishwazo inaendelea kukua. Awali, wasikilizaji wengi wa podikasti za Kiafrika walikuwa Waafrika walioko ughaibuni, lakini mwelekeo huu unabadilika kwa kuwa Waafrika zaidi wa nyumbani wanaendela kutambulishwa kwa chombo hiki.

Mipango ya kukusanya

Wakati janga lilipoufunga ulimwengu mwaka wa 2020, kanuni mpya zilizokuwa zimeandikwa zilitulazimisha kufutilia mbali tamasha yetu ya kwanza ya ana kwa ana ya Africa Podfest iliyokusudia kuwakusanya wanapodikasti kutoka Afrika yote pamoja na marafiki wa kupodikasti kwa Afrika kutoka ulimwenguni kote waliokuwa na msisimuko kama sisi.

Kubadilisha tamasha hilo kutoka la ana kwa ana hadi kwa mitandao huku tukiendele kulenga jamii na miungano kulituchochea kujenga mikusanyiko bora ya podikasti za mitandaoni.

Tunapoitazama historia ya kupodikasti katika Afrika, tutauona mwaka wa 2020 kama mwaka wa zinduzi kadhaa za podikasti za Afrika na ongezeko kubwa la mvutio katika upodikasti wa Afrika. Kazi kubwa na mabadiliko katika maisha ilimaanisha kwamba wazalishaji wengi wangetenga muda wa kubuni na kusimulia hadithi kupitia kwa podikasti.

Siku ya Podikasti ya Afrika ya kwanza ilizinduliwa tarehe 12 Februari 2020 kusherehekea kila kitu tunachokipenda kuhusu upodikasti kwa Afrika. Wanapodikasti wa Afrika waliikumbatia siku hiyo, na kuuhalalisha utafiti wetu wa awali (2018 hadi sasa) kuyazidi matarajio yetu. Kulikuwa na wanapodikasti na wapenzi wa upodikasti wengi zaidi ya tulivyofikiria.

Kadhalika, wasikilizaji wa podikasti walikuwa wakiitikia vyema maudhui kutoka kwa watunzi wa podikasti wa Afrika na kujiunga nao moja kwa mojamitandaoni, huku wakidai maudhui zaidi. Japo mwaka wa 2020 ulishuhudia ukuaji mkubwa ajabu katika umaarufu wa podikasti na utunzi wa podikasti, ulisaidia pia ukuaji wa utambulikanaji wa wanapodikasti wa Afrika katika jukwaa la kimataifa.

Kuanzia kwa uzinduzi wa mwanzo kabisa wa podikasti katika mataifa kadhaa ya Afrika hadi ongezeko muhimu katika podikasti za Kiafrika zilizojumuishwa katika mashindano hayo kama vile mpango wa utunzi wa Podikasti wa Google hadi kwa uzinduzi wa kivugulio cha upodikasti kilichofadhiliwa na BBC mapema 2021, kwa manufaa ya wanapodikasti wa Kenya, Nijeria na Afrika Kusini, mengi yamebadilika.

Wawili kati ya washindi watatu wa Afrika waliochaguliwa katika mpango wa watunzi wa Podikasti wa Google - podikasti ya ‘Letters to Boys’ (kutoka Nijeria) na ‘Contes et Légendes du Queeristan’ (kutoka Cameroon/Canada) – walianza kati ya mwezi wa Juni 2020.

Attendees Country Map: African podcasting is truly relevant to the rest of the world. These are the countries that the festival the attendees came from.
Wahudhuriaji Ramani ya Nchi: Podcasting ya Afrika ni muhimu kwa ulimwengu wote. Hizi ndizo nchi ambazo wahudhuriaji walitoka kwenye sherehe hiyo.

Bado, Changamoto

Licha ya hatua hizi, kupodikasti bado ni kugumu katika Afrika. Huku nyingi zikiwa zimefadhiliwa kutokana na hazina ya akiba ya kibinafsi, uzalishaji wa podikasti moja huwafilisisha wanapodikasti Waafrika, wengi ambao walikuwa na matarajio kwamba upodikasti utakuwa shughuli yao ya kiuchumi siku moja. Kwa mfano, uzalishaji podiksti moja unaweza kugharimu kati ya $1,000 kwa tukio moja hadi $12,000 kwa msururu mmoja wa matukio 12. Zaidi ya hayo, pia kuna gharama za kitaifa za usajili wa podikasti katika baadhi ya mataifa mbali na liseni za kila mwaka. 

Katika lugha na kanda mbalimbali, ufanisi wake finyu unakabiliwa na kodi mbalimbali ambazo ni mahususi kwa kila taifa, kanuni za udhibiti, na uwezo wa kupata umeme. Mtandao nafuu unatofautiana kutegemea taifa la Afrika wanamoishi.

Hata hivyo, waasisi wa kupodikasti wa Afrika wanakazana, huku wakizieleza vyema hadithi za Afrika (Inside Wants Out – podikasti ya mwelekeo Afrika kwa lugha asilia.), wanajitokeza kama wahifadhi wa historia (podikasti ya Zambia ya Leading Ladies) na kuwafanya Waafrika wasiokuwepo waonekane (podikasti za kijasusi Alibi – Afrika Kusini na Case Number Zero – Kenya). Huku misaada na tuzo zikitoa utambulisho muhimu unaohitajika zaidi pamoja na msaada wa kifedha, mengi yanaweza na yanastahili kufanywa.

Ukuaji wa jamii

Huku tukiwa tumechochewa na mapenzi yetu makuu ya kuileta jamii ya wanapodikasti wa Afrika, Africa Podfest na Podfest Cairo walikuwa wenyeji wenza wa utambulishaji (Roll Call) wa kwanza wa upodikasti wa Afrika kuwasalimia na kuwatambua wanapodikasti wa Afrika katika Siku ya Kimataifa ya Upodikasti ya mwaka jana taarehe 30 Septemba.

Tukiwa na mawasilisho ya washiriki kutoka kwa jamii zetu zilizojumuishwa, kuonana kupitia  utambulisho uliorekodiwa na wa moja kwa moja na utalii kulindaa jukwaa kwa ushirikiano wetu wa pili wa moja kwa moja mwezi wa Novemba ukiwa na kichwa Coping with COVID. Kupitia tajriba za wanapodikasti kutoka Angola, Nijeria, Misri, miongoni mwa mataifa mengine, tulitalii namna janga la COVI-19 lilivyochangia ukuaji wa upodikasti katika Afrika.

Kwa mfano, Pasha – podikasti kutoka Majadiliano Afrika (‘Pasha’ - a podcast from the Conversation Africa),  inatoa maelezo ya kiusomi kuhusu janga hili kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand nchini Afrika  Kusini. Tukio la maajuzi lilionyesha  programu mpya inayowasaidia wahudumu COVID wa mstari wa mbele kwa habari kuhusu afya ya akili (a new app which helps COVID-19 frontline workers with mental health).

 Kwa wasikilizaji wachanga, podikasti ya ‘Thandi and Captain Stay Safe’ inawalenga wahusika vibonzo walioundwa na jukwaa la Food For Mzansi, na inawafahamisha watoto wa Afrika Kusini kuhusu COVID-19. Mbali na hadithi yenye sehemu mbili ya watoto, watu wazima pia wanaweza kutarajia mahojiano ya waziwazi yatakayowasaidia kukabilia na kipindi cha janga hili.

Ubadilishanaji wa Maarifa ya Jamii

Tunaamini katika mikusanyiko ya kijamii ya kila mara na ya kawaida ambako tunazungumza na kusikilizana. Misururu ya Ana kwa Ana ya Tamasha zetu za Afrika za Upodikasti zimetutoa Johannesburg hadi Cairo huku ikiwawezesha wanapodikasti kuelezana kuhusu uelewa mahususi wa uchangamano wa kupodikasti wa kila taifa katika Afrika, ikiwa ni pamoja na umeme unaokatika kila mara, gharama za udhibiti, ukosefu wa msaada wa upodikasti na changamoto ya kudumisha uaminifu wakati kichochezi kikubwa ni mapenzi yako makuu, bali sio hundi. 

Miongoni mwa wanapodikasti waliohusishwa ni Jo Güstin, mtunzi wa Cameroon anayeishi Canada ambaye podikasti yake Contes et Légends du Queeristan, ni masimulizi ya kila wiki ya kifalsafa kuhusu watu wenye tabia mbadala za kiuana yasiyohusisha ashiki yanayowasaidia watu kulala na tabasamu nyusoni pao.

Mmisri Riham Jarjour (podikasti ya Rihamiat) alizungumzia tajriba yake alipoishi Lebanon, Syria, na Misri, ambazo zilileta mageuzi kwa podikasti yake ya kila wiki kwa Kiarabu kuhusu kuwa mama na mitindo ya maisha, kuzungumza wa hadhira pana ya Misri na nje.  

Kuubadilisha mchezo

Kuja pamoja kama wanapodikasti Waafrika kunatuonyesha namna sehemu kubwa ya kufanya sauti zetu zisikike kunahusisha kutengeneza podikasti na sauti anuwai pakubwa.

Ubunifu umekuwa sehemu kuu ya kila hatua ya upanuzi wa kupata huduma za kidijitali katika Afrika, na hili linawasaidia wanapodikasti Waafrika kukabiliana na changamoto wazipatazo – hasa katika mbinu za usambazaji.

Katika kutunga maonyesho mafupi ili kusambaza kirahisi katika WhatsApp (podikasti ya Africa Check’s anti-misinformation – What’s Crap on WhatsApp), kuchagua studio nafuu za kivugulio za upodikasti kama Sena Box ya Kenya na ujumuishwaji wa misimu, lugha asilia na kusimulia hadithi katika podikasti, tunaunda upya kielelezo  cha upodikasti katika Afrika.

More from this author