Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Kilimo kitasaidia au kuzamisha biashara huru ya Afrika

Get monthly
e-newsletter

Kilimo kitasaidia au kuzamisha biashara huru ya Afrika

Mageuzi katika mifumo ya kilimo na chakula yanaweza kufungulia uwezo wa Afrika
Abebe Haile-Gabriel
Afrika Upya: 
28 April 2021
Mtu aliye na mayai ya kuku mikononi mwake.
FAO
Eneo la Biashara Huria la Afrika linalenga kupanua biashara kati ya Afrika na kukuza ukuaji wa uchumi. Sekta ya kilimo inatoa msingi bora wa matarajio haya, anasema Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa FAO na Mwakilishi wa Kanda ya Afrika, Abebe Haile-Gabriel.

Eneo Huru la Biashara la Bara Afrika (AfCFTA) lina uwezo wa kuinua mamilioni ya watu kutoka umaskini na kumaliza upungufu wa chakula katika Afrika. Hata hivyo, ufanisi wake unategemea uidhinishwaji na utekelezwaji, na haswa katika sekta ya kilimo.

Abebe Haile-Gabriel
Bwana Abebe Haile-Gabriel, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi na Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Chakula na Kilimo Afrika la Umoja wa Mataifa.

Afrika inategemea mauzo ya bidhaa za kilimo kama kakao, kahawa, pamba, tumbaku na viungo kwa mataifa ya ulimwengu ili kupata fedha muhimu za kigeni. Lakini bara hili linaagiza vyakula muhimu kama nafaka, mafuta ya mboga, bidhaa za maziwa na nyama kwa kiasi kikubwa.   

Biashara kati ya mataifa ya Afrika katika bidhaa za kilimo kama asilimia ya jumla ya biashara ya Afrika ya kilimo imesalia chini ya asilimia 20 kwa muda mrefu, moja kati ya idadi ya chini kabisa katika kanda yoyote ile. Jumla ya biashara kati ya mataifa ya Afrika ilikuwa asilimia 2 pekee katika kipindi 2015–2017, ikilinganishwa na asilimia 67 kwa biashara kati ya mataifa ya Ulaya, asilimia 61 kwa mataifa ya Asia, na asilimia 47 kwa mataifa ya mabara ya Amerika, kwa mujibu wa shirika biashara la UN la UNCTAD.

 AfCFTA inakusudia kuibadilisha hali hii. Imeunda eneo huru la kibiashara lililo kubwa zaidi ulimwenguni, linalowakilisha soko la watejaa bilioni 1.2, na linayaagiza mataifa kuondoa vikwazo vya ushuru na visivyo vya ushuru ili kuimarisha usafirishwaji wa bidhaa na hudumu kati ya mataifa, na kuupiga jeki ukuaji wa kiuchumi katika kufanya hivyo.

Hata hivyo, tangu biashara ilipoanza chini ya AfCFTA tarehe 1 Januari 2021, ni mataifa 36 wanachama wa Umoja wa Afrika pekee yaliyoidhinisha makubaliano hayo. 

Umuhimu wa Kilimo

Ni katika kilimo ambako matumaini ya AfCFTA yanaweza kutimizwa, haswa kwa kuimarisha mikondo ya thamani ya kikanda iliyo jumuishi katika bidhaa zinazopewa kipaumbele, ikiongozwa na sekta ya kibinafsi yenye uanuwai na msukumo wa wafanyabiashara wadogo, wakulima wa kibiashara, wasimbaji pamoja na wahudumu.

Soko moja la Kiafrika lina uwezo wa kuunda mazingira bora, yenye ushindani zaidi wa biashara kwa kilimo, kuhamasisha uwekezaji zaidi na mwishowe sekta ya kilimo ya kisasa, yenye nguvu, yenye tija, inayojumuisha, endelevu na endelevu ambayo inaweza kuwaondoa mamilioni ya Waafrika kutoka kwenye umasikini.

Kuimarisha uwezo wa kitaifa wa uzalishwaji wa chakula na viunzi kwa masoko ya kikanda kutatoa msingi imara kwa mataifa kupiga jeki biashara ya kikanda. Sera na mipango inastahili kuhimiza sekta ya kibinafsi kuongeza uwekezaji mpya, kuongeza thamani kwa bidhaa , kushindana na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, na kubuni nafasi za ajira.

Mwelekeo wa Kikanda

Jumuiya nyingi za kiuchumi katika Afrika tayari zimetambua bidhaa za kimkakati kwa uboreshwaji zaidi katika mikondo ya kikanda ya kuongeza ubora:  Afrika Mashariki imeupa kipaumbele mchele, maharagwe na bidhaa za maziwa miongoni mwa nyingine. Afrika Magharibi imeyapa kipaumbele mawele, mifugo, samaki na bidhaa za majini, miongoni mwa nyingine. Bidhaa zilizopewa kipaumbele Kusini mwa Afrika ni soya na njugu.

Mwelekeo huu wa kikanda una uwezo wa kuwajumuisha wakulima wadogowadogo ikiwa ni pamoja na wanawake na vijana, pamoja na biashara ndogu na za wastani, na kuwaunganisha kwa sekta kuu ya kibinafsi inayotawala masoko ya pembejeo na mazao.

Ujumuishwaji ulioimarika wa washikadau katika mikondo ya thamani ya kibiashara, kuanzia wakulima na wasimbaji, wasafirishaji na wauzaji, unaweza kubuni nafasi endelevu za ajira na kuimarisha uzalishawaji ulioimarika kwa kipindi kirefu, na usiodhibitiwa na wakati, utoshelevu wa chakula na lishe.

Katika Mwaka huu wa Kimataifa wa Matunda na Mboga, ushuru uliopunguzwa kwa vyakula vibichi pamoja na kuondolewa hatua kwa hatua kwa vikwazo visivyo vya ushuru kunaweza kuwafanya watu wengi Afrika waweze kumudu vyakula vya aina nyingi na vyenye lishe bora - uchanganuzi wa hivi karibuni wa FAO unaonyesha kwamba karibu watu bilioni moja katika bara Afrika hawawezi kumudu lishe bora.  

Jamii nyingi za kiuchumi za bara tayari zimegundua bidhaa za kimkakati kwa maendeleo zaidi katika minyororo ya thamani ya kikanda: Afrika Mashariki imepeana kipaumbele kwa mchele, maharagwe na maziwa, kati ya mengine. Afrika Magharibi imetoa kipaumbele kwa mtama, mifugo, samaki na mazao ya samaki. Vipaumbele vya Kusini mwa Afrika ni pamoja na maharage ya soya na karanga.

Kuubadilisha mwelekeo kutoka kwa kawaida

Ongezeko la biashara kati ya mataifa ya Afrika ni badiliko la mwelekeo kutoka hali ya kawaida. Ufanisi wa eneo huru la biashara kubwa zaidi ulimwenguni unategemea serikali na sekta ya kibinafsi. 

Mataifa na kampuni zinakabiliana na vikwazo vikuu kama vile kushughulikia kanuni zinazokinzana za asili na usalama wa chakula na mahitaji ya kubandika alama za utambulisho, na zinastahili kushinda miundomsingi duni kama mawasiliano ya simu na mifumo ya barabara, na haja ya taarifa bora kuhusu masoko.

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika maajuzi liliuzindua utaratibu wa kuyasaidia mataifa katika kujirekebu kwa soko moja jipya.

Lengo moja kuu la (utaratibu huo) Framework for Boosting Intra-African Trade in Agricultural Commodities and Services ni kuyasaidia mataifa kuongeza biashara kati yao mara tatu katika bidhaa na huduma za kilimo ambalo ni miongoni mwa mambo ambayo serikali za Afrika zilijitolea kufanya chini ya azimio la Malabo lililoidhinishwa mnamp 2014 (Malabo Declaration adopted in 2014).

Kuwezesha sekta madhubuti ya kibinafsi ni hatua muhimu ya mapema, kwa kuwa biashara ndogo hadi za wastani ni muhimu katika mageuzi ya kimuundo ya mifumo ya kilimo na chakula katika Afrika.

Serikali zinastahili kubuni mifumo ya wanunuzi na wagavi, ikiwaunganisha wazalishaji wadogo na wa wastani, ikiwa ni pamoja na wakulima wadogowadoga, kwa wanunuzi ndani ya mataifa na kikanda. Wanawake na vijana wanastahili kujumuishwa katika juhudi hizi.

Mabadiliko kutoka kwa mifumo ya uzalishwaji chakula cha matumizi hadi mifumo ya bora, jumuishi, nyumbufu na endelevu ya kibiashara yanahitaji kuboreshwa katika uzalishwaji wa kiwango cha shambani, pembejeo, matumizi ya mashine na usimamizi wa baada-mavuno ukiongozwa na uwekezaji, teknolojia, ubunifu na maarifa asilia.

Inakadiriwa kwamba kuweka huru ushuru kunaweza kuleta manufaa ya ustawi wa hadi $ bilioni 16.1, na ukuaji wa biashara kati ya mataifa ya Afrika wa asilimia 33.

Tunapotazama mbele, soko moja la Afrika linaweza kubuni mazingira ya ushindani zaidi wa kibiashara kwa kilimo, kuhimiza uwekezaji zaidi sekta ya kisasa, yenye msukumo, zalishi, jumuishi, nyumbufu na endelevu ya kilimo kinachoweza kuinua mamilioni ya Waafrika kutoka kwa umaskini.

Bi.  Haile-Gabriel ni Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mwakilishi wa Kikanda wa Afrika kwa Shirika la Chakula na Kilimo la UN

Abebe Haile-Gabriel
More from this author