Kutana na Mabingwa wa Chakula Barani Afrika

Get monthly
e-newsletter

Kutana na Mabingwa wa Chakula Barani Afrika

Kabla ya Mkutano wa Mifumo ya Chakula wa 2021 wa UN mnamo Septemba hii, Mabingwa wa Mifumo ya Chakula wanakusanya jamii za ulimwengu na kukuza mazungumzo kwa suluhisho za ubunifu, vitendo na endelevu.
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
9 June 2021
Divine Ntiokam, Lucy Muchoki Mike na Nkhombo Khunga
Divine Ntiokam, Lucy Muchoki Mike na Nkhombo Khunga.

Baada ya mchakato mrefu na mpana wa ushauri hatimaye, Jamii ya ulimwengu itakutana mnamo Septemba 2021 kukagua mifumo ya chakula ulimwenguni kwenye Mkutano wa Mifumo ya Chakula wa Umoja wa Mataifa wa 2021.

Katika miaka miwili ya maandalizi ya Mkutano huu, kote ulimwenguni watu wamepata fursa ya kutoa maoni yao, kubadilishana maoni na kutoa suluhisho katika juhudi za pamoja za kubadilisha njia tunazotumia kukuza, kula na kudhibiti vyakula vyetu tunapoelekea hali endelevu.

Shirika la Umoja wa Mataifa lilizindua Mabingwa wa Mifumo ya Chakula - kikundi anuwai cha watu wanaotambuliwa katika jamii zao na nyanja zao za kazi - kuhamasisha jamii za ulimwengu na kuendeleza mazungumzo ambayo yanalenga kupata masuluhisho yenye ubunifu na yanayotekezeka. Uzinduzi huu ulikuwa juhudi za  "kuhakikisha Mkutano wa Mifumo ya Chakula unapata maoni mengi ya washiriki katika mifumo ya chakula," alisema Bi Agnes Kalibata, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Mkutano wa Mifumo ya Chakula, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huu.

Kikundi cha kwanza cha viongozi katika nyanja zao na jamii watatetea mifumo thabiti zaidi ya chakula, yenye afya, inayojumuisha na endelevu. Watahamasisha muungano wao ili kushiriki katika mazungumzo na kuleta hatua za kuwezesha masuluhisho yanayoweza kufikiwa na mapana ili kushinda changamoto katika mifumo ya chakula ya kitaifa na kikanda.

Mabingwa wa Mifumo ya Chakula wanajumuisha viongozi wa vijana na watu wa asili, wakulima wadogo na wanasayansi kutoka kote ulimwenguni, pamoja na wakuu wa lishe, afya, hali ya hewa, maumbile, jinsia, sera pamoja na jamii zinazohusiana na uzalishaji, wakademia, biashara, fedha na teknolojia.

Mabingwa hawa watashirikiana kwa karibu na Bi. Kalibata, kuanza shughuli katika kujiandaa kwa Mkutano huu, pamoja na majadiliano kuhusu jinsi ya kuchochea na kujenga muungano wao ili kuanzisha hatua mpya, masuluhisho bunifu, na mipango ya kubadilisha mifumo ya chakula kambatana na miktadha anuwai ya nchi.

"Kikundi hiki cha kusisimua na anuwai cha viongozi kitaanzisha Muungano wa Mabingwa wa Mifumo ya Chakula ili kuhakikisha Mkutano wa Mifumo ya Chakula unafaidi kwa maoni mengi na yenye kina ya wahusika katika mifumo ya chakula," Bi. Kalibata alisema.

"Muungano huu utakuwa nguzo muhimu ya Mkutano Mkuu katika miezi ijayo, na utakuwa katika mstari wa mbele wa harakati mpya ya kubadilisha mifumo ya chakula ulimwenguni kuwa bora."

Baada ya miezi michache tu katika kazi yao, Afrika Upya ilipatana na Mabingwa watatu wa Chakula walioko barani Afrika - Bwana Divine Ntiokam wa Kamerun, ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, Muungano wa Vijana katika Kilimo Bora kwa Hali ya Hewa (CSAYN); Bi. Lucy Muchoki wa Kenya, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji, Muungano wa Afrika katika Kilimo-Biashara na Sekta ya Kilimo (PanAAC) na Bwana Mike Nkhombo Khunga wa Muungano wa Asasi ya Kiraia kuhusu Lishe (CSONA) nchini Malawi, kusikia tajriba zao za kibinafsi kama wanachama wa Muungano huu na jinsi inavyohisika kuwa sehemu ya mazungumzo ya ulimwengu. Tazama masimulizi yao yanayofuata: