Bingwa wa Mifumo ya Chakula Mike Khunga, Malawi

Get monthly
e-newsletter

Bingwa wa Mifumo ya Chakula Mike Khunga, Malawi

Muungano wa Asasi za Kiraia za Lishe (CSONA), Malawi
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
9 June 2021
.
Mike Nkhombo Khunga
Mike Nkhombo Khunga

Je, inahisije kuwa Bingwa wa Chakula wa Umoja wa Mataifa?

Ni tajriba ya kushangaza kutambuliwa kama bingwa kwa sababu ya kazi yako. Inakuweka kwenye mazungumzo na mashirikiano mengi, ambapo unapata utaalamu mwingi katika kukuza masuluhisho, uratibu na maoni ya kuendeleza mifumo ya chakula. Tajriba inakuwa nyingi kwa sababu ya fursa unazopata.

Hapo awali, matarajio yangu yalikuwa kwamba Umoja wa Mataifa ungenilipa kwa kuwa Bingwa wa Chakula, lakini ndipo nikagundua kuwa ni jambo la mapenzi kwa watu masikini na mafukara. Hata bila kulipwa, unafanikiwa sana kwa kushiriki katika kuunda masuluhisho yanayolenga watu masikini.

Maono yangu yamekuwa makubwa sana, na yamenipeleka kwenye mikutano na majukwaa kadhaa. Nimekuwa na fursa za kutangamana na watu kutoka nyanja kadhaa za utaalamu, ambapo nimejifunza mambo mengi.

Kuna mambo mabayo hukuyatarajia, mazuri au vinginevyo?

Nimeweza kuongoza mikutano kadhaa ya ulimwengu na nimekuwa katika jopo na watu wengi ambao sikuwahi kufikiria nitawahi kushiriki nao katika jukwaa moja. Nimetagusana na David Nabarro [Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkutano wa Chakula] na pia Agnes Kalibata [Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Mkutano wa Mifumo ya Chakula] na nimetambuliwa kama kijana anayefanya mengi barani Afrika. Nimekuwa na fursa za kuchangia mawasiliano ya Umoja wa Mataifa kupitia blogi zangu.

Je,  ulianza utetezi kuhusu chakula lini?

Ninaongoza kundi la vijana kwenye Hatua ya Vitendo 5 [Kujenga uhimilivu katika hali ngumu, majanga na mifadhaiko] mimi ni naibu mwenyekiti. Mimi ni nguzo kwa makundi mengi ya vijana kuhusu mageuzi ya Mfumo wa Chakula wa Umoja wa Mataifa. Ninawashauri vijana wengi kuwa na mazungumzo huru na nimeweza kuunganisha vijana kutoka nchi dhaifu na zenye mizozo na Hatua ya Vitendo 5.

[Hatua za Vitendo za Mkutano wa Mifumo ya Chakula zinawapa wadau kutoka usuli mbalimbali nafasi ya kushiriki na kujifunza, kwa nia ya kukuza vitendo vipya na ushirikiano na kuendeleza mikakati iliyopo. Hatua za Vitendo zinawiana na malengo matano ya Mkutano. Kila Hatua ya Vitendo imeundwa kushughulikia uwiano unaowezekana na hatua zingine, na kutambua suluhisho ambazo zinaweza kuleta faida nyingi.]