Ukuzaji viwanda jumuishi na endelevu ni muhimu kwa ufanifu wa Afrika

Get monthly
e-newsletter

Ukuzaji viwanda jumuishi na endelevu ni muhimu kwa ufanifu wa Afrika

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN Siku ya Afrika ya Ukuzaji Viwanda
Secretary-General António Guterres
Afrika Upya: 
20 Novemba 2021
 António Guterres
UN Photos
Katibu Mkuu wa UN António Guterres

Tatizo la COVID-19 linaendelea kuziathiri vibaya chumi na jamii kote.

Wakati uo huo, uwekezaji katika ukombozi baada ya janga ni fursa ya kizazi kufanya mageuzi jasiri na kuchukua hatua za kasi kutimiza Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu, kuuangamiza umaskini, kuondoa tofauti za kiuchumi na kukuza unyumbufu wa tabianchi.

Mustakabali wa ufanisi wa bara Afrika umekitwa katika kuzipanua fursa kwa wanawake na wasichana, kuwekeza katika vijana, kuendeleza mageuzi ya kilimo na ya kiviwanda na ukuaji uliowajibika na fanifu wa kiviwanda kupitia uhamishaji wa teknolojia, ubunifu na ushirikiano, na utekelezwaji kikamilifu wa Mkataba wa Soko Huru la Afrika.

Maendeleo jumuishi na endelevu ya kiviwanda na uanuwai wa kiuchumi huwezesha ukuaji na maendeleo kupitia kujitegemea na kupunguza utegemezi kwa chumi za kimataifa.  Ni muhimu hata zaidi katika ulimwengu usio na umoja na changamoto nyingi za kimataifa – kuanzia kwa ukosefu wa usawa katika chanjo na tofauti za kidijitali.

Katika Siku ya Afrika ya Ukuzaji Viwanda, ninakariri kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kushirikiana na viongozi na watu wa Afrika kuufanya ukuaji wa viwanda jumuishi na endelevu njia bora ya kufika bara fanifu na lenye amani.