Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Tohara za wanaume zavurugwa na COVID-19, zakosa kutimiza shabaha ya 2020

Get monthly
e-newsletter

Tohara za wanaume zavurugwa na COVID-19, zakosa kutimiza shabaha ya 2020

Afrika Upya: 
1 December 2021
Na: 

Katika maeneo yaliyo na mweneo mkuu wa VVU na viwango vya chini vya tohara, Tohara Tiba ya Hiari (VMMC) yaweza kuchangia pakubwa uzuiaji wa VVU.

Licha ya haya, idadi ya Tohara Tiba za Hiari zilizotekelezwa katika mataifa 15 ya kipaumbele ilipungua mwaka 2020, hasa kwa sababu ya kuvurugwa kwa huduma kulikosababishwa na janga la COVID-19: takriban tohara milioni 2.8 zilifanywa 2020, ikilinganishwa na milioni 4.1 mwaka 2019.

Mataifa kadhaa yalisimamisha mipango yake wakati janga hilo lilipokita mizizi, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini.  Licha ya hayo, mipango katika mataifa mengine ilikuwa nyumbufu kiasi cha kurejelewa upesi na kupanuliwa katika miezi ya mwisho ya 2020—hasa nchini Rwanda na Zambia, ambako mpango huo uliimarika kwa takribani 15%. 

Katika mataifa haya, marekebisho ya kuendeleza huduma za VMMC katika kipindi cha COVID-19 yalijumuisha mabadiliko katika utangazaji na uzalishaji wa utashi, usafirishwaji wa wateja, kutolewa kwa huduma katika kituo cha afya au ndani ya jamii na miadi ya ufuatilizi baada ya tahara.

Jumla ya VMMC milioni 18 zilifanywa katika kipindi 2016–2020, mbali kabisa na shabaha ya 2020 ya milioni 25.

Mbali na COVID-19, pingamizi nyingine mwaka 2015 na 2016 ilikuwa ugunduzi wa visa vya  pepopunda nchini Uganda, ambayo ilisababisha kupunguzwa kwa shughuli nchini humo.