COP26: Mkataba muhimu wa dola milioni 500 wazinduliwa kuulinda msitu wa DRC

Get monthly
e-newsletter

COP26: Mkataba muhimu wa dola milioni 500 wazinduliwa kuulinda msitu wa DRC

Kupotea kwa msitu katika DRC kunakuzwa na ufukara uliokithiri, haswa kwa sababu ya ongezeko la watu wasio na vitekauchumi
Afrika Upya: 
2 Novemba 2021
Na: 
Msitu mnene.
CAFI
Ikichochewa zaidi na umaskini uliokithiri, upotevu wa misitu nchini DRC unatokana zaidi na ongezeko la watu wanaokosa fursa za kujikimu nje ya msitu na kutegemea zaidi kuni kupikia.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 

Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Waziri Mkuu Boris Johnson wa Uingereza kwa niaba ya Mpango wa Msiti wa Afrika ya Kati (CAFI) juma lililopita waliuunga mkono makataba muhimu wa miaka 10 (2021-31)  kuulinda Msitu wa Bonde la Kongo – wa pili kwa ukubwa ulimwenguni.

  • Msitu wa DRC unawakilisha 10% ya misitu kwenye maeneo ya joto ulimwengu. Chemichemi zake zinakalia eneo la kilomita 100,000 mraba na ndizo kubwa zaidi ulimwenguni. Mfumoikolojia wake unatoa huduma ya kubwia kaboni sawia na miaka 10 ya itolewayo kimataifa.  Ahadi nyingi zinazojitokeza katika Barua mpya ya Kusudi zinadhihirisha kujitolea kwa kiwango cha juu cha DRC kuanzisha uchumi safi unaokitwa katika uharibifu wa chini kabisa wa misitu.
  • Huku ikisaidiana na mataifa ya Ulaya, Jamhuri ya Korea, Jumuiya ya Ulaya na Uingereza na Ireland Kaskazini, Mpango wa Msitu wa Afrika ya Kati  (CAFI) ni Hazina ya Umoja wa Mataifa na ukumbi wa mazungumzo ya kisera unaolenga kuyasaidia mataifa sita ya Afrika ya Kati kupata njia ya maendeleo yanayohusu utoaji wa kiwango cha chini cha kaboni zinazohakikisha ukuaji wa kiuchumi na kupunguza umaskini huku zikilinda misitu na mali asilia ambazo watu wanategemea.
  • CAFI kwa hivyo inajumuisha uwekezaji na mazungumzo ya hali ya juu kuhusu sera ili kuyasaidia mataifa sita washirika kuutekeleza Mkataba wa 2015 wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kukabiliana na umaskini na kupata maendeleo endelevu huku yakizingatia mfumo wa uanuwai-viumbe wa baada-2020.
  • Msitu wa maeneo ya joto wa Afrika ya Kati unakabiliwa na shinikizo. Huku mikondo na sababu zikitofautiana mno katika mazingira ya kila taifa, kupotea kwa msitu kunawakilisha ekari milioni 6 ya msitu maeneo la joto tangu 2001, sawia na viwanja milioni 6 vya raga.
  • Huku ukiwa makao ya zaidi ya spishi zaidi ya 10,000 ya wanyama na mimea, nyingi yazo zisizopatikana kwingineko, msitu wa Afrika ya Kati ni tegemeo muhimu la chakula, kawi, makazi na masuala ya kiroho katika baadhi ya mataifa yenye viwango vya chini mno vya maendeleo ya kibinadamu na idadi kubwa ya watu wenye haja ya msaada wa dharura wa utoshelevu wa chakula ulimwenguni.
  • Bonde la Kongo ni moja kati ya maeneo ya mwisho ulimwenguni kubwia kaboni vyingi kuliko inayoitoa. Msitu wake, wa pili kwa ukubwa ulimwenguni, unabwia  karibu bilioni 1.5 ya CO2 kutoka angani kila mwaka au 4% ya toleo la kimataifa.

Mkataba huo utavutia wafadhili wengi wenye uwekezaji wa dola million 500 za Marekani kwa miaka mitano ya kwanza.

“Kwa misitu yake, maji na raslimali za madini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni "Taifa la Suluhisho" la dhati kwa tatizo la tabianchi. Ili kuilinda misitu yetu na kuukuza usimamizi wake endelevu, kipaumbele chetu kilichopigwa jeki na huu ushirikiano mpya ni kuimarisha utawala na uwazi katika sekta zote za matumizi ya ardhi. Ushirikiano huu pia utaisaidia ari yetu kuwajibikia changamoto mbili za utoshelevu wa chakula na mabadiliko ya tabianchi kupitia kilimo endelevu, haswa katika maeneo ya savana”, alisema rais Tshisekedi.

Sekta zote za uchumi wa DRC zimejiunga na mkataba huu muhimu kufanya matendo yanayoweza kubadilisha desturi za kutumia ardhi zilizodumu kwa milenia. Hizi juhudi za pamoja ni muhimu katika nchi inayotoshana na Ulaya Magharibi na yenye mojawapo ya viwango vya chini kabisa vya maendeleo ya kibinadamu, na inayopoteza karibu ekari nusu milioni ya msitu kila mwaka.

Kupitia ushirikiano huu mpya wa miaka mingi, DRC inalenga kwanza kudhibitia kuisha kwa msitu kwa wastani wake wa 2014-2018 na kuhakikisha kwamba uharibifu wa misitu unaendelea kupungua. Ushirikiano huo pia utasaidia ukuzaji upya wa ekari milioni 8 za ardhi na misitu iliyoharibiwa, na na kuweka 30% ya maeneo ya kitaifa katika hali ya ulinzi, ikiwa ni pamoja na maeneo ambako jamii asilia zinafanya juhudi za kusimamia misitu kwa njia endelevu.

Bwana Goldsmith, Waziri wa Uingereza wa Pacific na Mazingiara alitangaza: “Uingereza ina fahari kuyatia sahihi makubaliano haya ya miaka kumi kwa pamoja na Mpango wa Misitu wa Afrika ya Kati pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hii ni hatua muhimu mbele katika juhudi zetu kulinda na kuirejesha misitu ya thamani ya taifa hili, pamoja na kuweka vitekauchumi ndelevu na kupunguza umaskini."

Huku kukizidishwa na ufukara, kupotea kwa msitu DRC kunatokana haswa na ongezeko la watu wasio na fursa za vitekauchumi nje ya msitu na kutegemea kuni kwa upishi, haya yote yakitokea katika mazingira ya kukosa mpango wa matumizi ya ardhi. Suluhisho lolote linlopendekezwa kukabili kupotea kwa msitu katika DRC kwa hivyo linastahili kulenga maendeleo mashambani, kupunguza umaskini na kuimarisha utoshelevu wa chakula.

Msaada wa CAFI wa $ milioni 500 kwa miaka ya kwanza mitano ni zaid ya maradufu ya $ milioni190 zilizotolewa chini ya Barua ya Kusudi ya kwanza (2015-2020), ambayo malengo yake yaliwasilishwa kupitia stakabadhi za karibu mipango ishirini  ambayo ilisaidia mageuzi ya kiwango kikubwa katika kilimo, mipango ya matumizi ya ardhi na umilikaji; ikaelekeza shughuli za kilimo kwa mamia ya maelfu ya ekari ya savana; na ikaimarisha vitekauchumi vya mamia ya maelfu ya watu. 

Tangazo katika COP26 linahitimisha miezi ya majadiliano kati ya CAFI na wadhamini na mawaziri wa DRC, ambamo makundi ya uraia ya kitaifa yalihusika kikamilifu. Katika taarifa, Guy Kajemba, Mshirikishi wa kitaifa wa muungano wa makundi ya uraia “Groupe de Travail Climat REDD+ Rénové” alitangaza:

"Tunaukaribisha huu ushirikiano uliofufuliwa. Utatusaidia kuchunguza ahadi zilizotolewa, ikiwa ni pamoja na hatua zitakazoelekeza kwa kuondolewa kibali kwa njia ya uwajibikaji na taratibu, uchapishaji wa mikataba katika sekta zote zinazohusiana na matumizi ya ardhi na ahadi iliyotolewa na rai Tshisekedi kubatilisha kandarasi zote ghushi za kibali.  Tunahimizwa haswa na maandalizi ya sekta zote zinazojitolea kuilinda Misitu ya Thamani Kuu na chemchemi.”

MALENGO 12 THABITI YA BARUA YA KUSUDI YA DRC-CAFI 2021-2031

  1. Misitu ya thamani kuu, chemchemi na kibali cha jamii kwa msitu yanaanza kujumuishwa taratibu katika mipango ya matumizi ya ardhi, kwa lengo la kudumisha dhima yake muhimu.
  2. Kiwango cha kawi ya miti isiyo endelevu (kama makaa) ya kupikia kipunguzwe kwa nusu katika maeneo ya miji (angalizo: 97% ya wakazi milioni 13 wa Kinshasa wanatumia kawi ya miti kila siku kwa upishi na wanatumia zaidi ya tani 17% ya miti kwa mwaka, ambayo kwa pakubwa inapatikana kwa njia isiyo endelevu.
  3. Hakuna kibali cha viwanda vitegemeavyo kilimo kitakachotolewa katika misitu ya thamani ya juu chemchemi.
  4. Uwazi katika usimamizi wa mali asilia unaimarishwa kupitia mageuzi ya kisheria kibali cha kilimo kilichoko, ukataji miti, madini na mafuta, kubatilisha kile haramu, pamoja na kuchapisha kandarasi zote (zinazohusiana na the Extractive Industries Transparency Initiative - EITI).
  5. Hatua wazi za ugavi zinazingatiwa katika kutoa kibali cha kilimo na ukataji miti.
  6. Usimamizi wa misitu unaimarishwa kupitia kwa udhibiti thabiti na ekari milioni 5 zilenge ukuzaji msitu wa jamii, huku ikiongeza maradufu shabaha ya awali ya kitaifa, pamoja na kuweka mfumo wa kisheria na wa udhibiti ili kulinda haki za watu asilia. Sahihi ya tangazo la kuondolewa kwa kibali itatiwa tu baada ya kutimiza mipango ya kijiografia ya ugavi wa siku za usoni kwa kuzingatia mchakato wa mashauriano.
  7. Kulingana na ahadi ya 30 x 30 ya kimataifa, DRC inatoa 30% ya nchi kuwa chini ya ulinzi wa aina mbalimbali kufikia 2030 huku ikiheshimu kuweka huru kibali na uelewa wa awali na kuhakikisha sauti za jamii zilizotengwa zinasikika. Hili litajumuisha maeneo ambayo jamii zenyewe zinatoa kwa ulinzi kupitia mchakato wa ugavi kieneo zinazouongoza.
  8. Ekari milioni nane ya ardhi na misitu iliyoharibiwa itakombolewa, kulingana na ahadi ya DRC chini ya Changamoto ya Kimataifa ya Bonn kuhusu ukombozi wa mandhari yaliyoharibiwa na misitu kuangamizwa.
  9. Sheria na sera mpya bunifu ya umiliki zinakubaliwa na kutekelezwa, pamoja na kuwasilishwa kwa mfumo wa habari iliyogatuliwa inayojumuisha sajili za umiliki za kiwango cha kijamii.
  10. Viwango vya ubora vya kijamii na kimazingira vipya vinatekelezwa ili kupunguza athari za uchimbaji madini na uwekezaji wa mafuta katika misitu na uanuwai wa viumbe, pamoja na hatua zilizoimarishwa katika maeneo ya misitu ya thamani ya juu na chemchemi. Shughuli zozote zisizokubaliana na malengo ya uhifadhi katika maeneo yaliyolindwa zinapigwa marufuku.
  11. Sera ya kitaifa kuhusu idadi ya watu inayozingatia haki, kuongozwa na ushahidi na kujali usawa wa kijinsia inatekelezwa kupiga jeki mpito wa kidemografia ambayo inachochea ukuaji wa kiuchumi na kufikia malengo ya maendeleo.
  12. Eneo maalumu kielelezo cha uchumi wa misitu lifanyiwe majaribio ili kusaidia uchumi safi wa uharibifu wa misitu wa kiwango cha chini, na kuzingatia misitu ya thamani ya juu, chemchemi na michkato ya kupanga ardhi.
Mada: 
More from this author