Pata programu za rununu za bure

Pata habari mpya kutoka kwetu kwenye programu zetu.

Download app from Android Download app from Apple

Jinsi Umoja wa Mataifa unavyopanua nafasi za biashara za Bara Afrika

Get monthly
e-newsletter

Jinsi Umoja wa Mataifa unavyopanua nafasi za biashara za Bara Afrika

— Christian Saunders
Kingsley Ighobor
Afrika Upya: 
7 August 2019
Christian Saunders, UN Assistant Secretary-General, Supply Chain Management
Christian Saunders, Katibu Mkuu Msaidizi ─ Usimamizi wa Mfumo wa Ununuzi.

Christian Saunders, ndiye Katibu Mkuu Msaidizi  wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya Usimamizi wa Mfumo wa Ununuzi. Yeye hutoa usaidizi wa kitaasisi kwa ofisi za nyanjani za Umoja wa Mataifa, ikiwemo misheni za kulinda amani barani Afrika. Huku akiongoza mageuzi kuimarisha ufaafu wa mfumo wa ununuzi, Bw. Saunders angependa kuona kampuni nyingi za Afrika zikifanya biashara na Umoja wa Afrika ambao malengo yake ya ununuzi yana thamani ya mabilioni ya dola za kiMarekani. Je, Biashara za Afrika zinalazimika kufanya nini ili kushinda zabuni zinazotolewa na Umoja wa Mataifa? Je, kuna nafasi kwa wafanyabiashara wanawake kutoka Afrika? Katika mahojiano haya na Kingsley Ighobor, kutoka Afrika Renewal, Bw. Saunders anajibu maswali haya na kuwasilisha matumani yake kwa mustakabali wa uchumi na jamii ya Afrika.  Hizi hapa ni sehemu fupi za mahojiano.

Afrika Renewal: Duniani kote, Umoja wa Mataifa umekuwa ukigeuza usimamizi wake wa mfumo wa ununuzi. Je, hii inatarajiwa kukuza ufanisi vipi, haswa katika misheni ya nyanjani yenye makao mengi Afrika?

Christian Saunders: Wakati Katibu Mkuu António Guterres alichaguliwa kuongoza Umoja wa Mataifa, aligundua kuwa shirika hili lilihitaji kutumia mbinu za kisasa, kupunguza umangimeza wake, kugatua mamlaka, na kubadilisha mazoea yake ili kulenga "matokeo na watu badala ya umangimeza na michakato." Hii ni pamoja na mfumo wake wa ununuzi; Kuunyoosha na kuufanya kukidhi matakwa. Alitambua pia haja ya kuwapa watu wanaofanya kazi nyanjani, haswa katika operesheni za kudumisha amani, usaidizi bora wa kutelekeza wajibu wao kwa ufanisi.  Mageuzi haya yangekuza ufanisi katika shirika nzima.

Kwa hiyo, kuna athari gani kufikia sasa?

Mageuzi haya ya Usimamizi ya Katibu Mkuu na mabadiliko katika mfumo wa ununuzi yalizinduliwa mnamo Januari mwaka huu, kwa hiyo bado tuko katika siku za mwanzo za mageuzi yenyewe. Kama sehemu ya Ofisi mpya ya Usimamizi wa Mfumo wa Ununuzi, tuliunganisha ununuzi na mipango ya usafiri — awali zilikuwa katika idara tofauti — kuwa katika mfumo unganishi wa ununuzi chini ya Idara ya Usaidizi wa Operesheni. Sasa, kama kitengo kimoja, tunalingana  zaidi na matakwa. Sasa tumenyooka zaidi. Je,  kazi imekamilika? La, bado. Bado tuna hatua kadhaa kutimiza, lakini tuko njiani katika kuboresha usaidizi tunaotoa kwa operesheni za kudumisha amani. Kwa mfano, tuko katika mchakato wa kutia saini kandarasi za muda mrefu za kusafirisha mizigo mwezi huu. Hili litafanya uchukuzi kuwa rahisi sana kwa misheni zetu za kudumisha usalama.

Sehemu ya agenda ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake. Kwa kuwa ukubwa wa Mfumo wa ununuzi wa Umoja wa Mataifa ni karibu dola za Marekani bilioni 17 — zaidi ya Pato la Kitaifa la mataifa mengi ya Afrika — ofisi yako inawawezeshaje wanawake wa Afrika wanaotaka kufanya biashara na Umoja wa Mataifa?

Mimi ni mkeretekwa mkuu wa usawa wa kijinsia. Nafikiri usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ni suala ambalo limepuuzwa kwa muda mrefu. Katika mfumo wetu wa ununuzi wa Umoja wa Mataifa, tunafanya kazi kuhakikisha kuwepo kwa nafasi, haswa kwa biashara ndogo na za kati zinazoendeshwa na kumilikiwa na wanawake wa Afrika na mataifa mengine yanayostawi. Wanawake wanahimizwa kuomba zabuni za Umoja wa Mataifa.

Je,  wanawake hawa wanaomiliki biashara wanatakiwa kufanya nini?

Umoja wa Mataifa hununua bidhaa na huduma nyingi kuliko shirika lingine lolote kwa kuwa hununa bidhaa tofauti zipatazo 60,000.  Kwa hivyo, kuna nafasi kubwa kwa biashara aina tofauti, kubwa na ndogo, za kuuzia Umoja wa Mataifa. Sisi hununua bidhaa kama vile vifaa vya kuandikia, vyakula, Teknoloji ya habari, mafuta, magari ya silaha, huduma za anga na zingine nyingi.

Je, ili kushinda kandarasi za Umoja wa Mataifa, ni lazima wanunuzi wawe mashirika makubwa ya kimataifa?

La, hayo ni mawazo potofu. Wauzaji wengi, hasa wafanyabiashara ndogo, huogopa kufanya biashara na Umoja wa Mataifa na labda hufikiria, "Aah, hili ni shirika kubwa la New Yorkni vigumu kwetu kufanya biashara na Umoja wa Mataifa." Lakini ukweli ni kwamba idadi ya maagizo yetu ya ununuzi yako chini ya $ 50,000. Maadam wanaweza kuuza tunachohitajikwa kazi kidogo ya ziada na uvumilivu—kampuni nyingi ndogo na za kati zinaweza kufanya biashara na Umoja wa Mataifa.

Je, nini maoni yako kuhusu uhusiano wako na biashara bara Afrika kwa sasa?

Mwaka jana tulishirikiana na kampuni kutoka nchi 54 za Kiafrika kwa biashara ya jumla ya dola milioni 600 katika bidhaa na huduma tofauti—mafuta, ujenzi, upishi, chakula, teknolojia ya mawasiliano, huduma za anga, na kadhalika.

Hii inamaanisha kuwa unafanya biashara na nchi nyingi—sio tu na nchi ambazo una misheni kubwa ya kudumisha amani?

Tunafanya biashara na bara zima ingawa ni wazi,  kuwa katika nchi hizo zenye shughuli za kudumisha amani huwa tunafanya biashara nyingi.

Je, unaendeleza vipi shughuli zako ili kuridhisha wateja wako wasiojua umangimeza?

Wakati Katibu Mkuu alipokuwa anatoa mageuzi ya usimamizi wake, moja ya vipaumbele vyake ni kuboresha na kurahisisha umangimeza wa Umoja wa Mataifa—ili iwe rahisi kwa watu kufanya kazi fulani, na pia kwa washirika kufanya biashara na Umoja wa Mataifa. Ndio, tuko katika mchakato wa kurahisisha taratibu zetu za ununuzi ili kuwezesha wauzaji kupata ufikiaji rahisi wa Umoja wa Mataifa. Sasa, badala ya kujisajili kufanya biashara na kila shirika (Umoja wa Mataifa una mashirika mengi), unaweza kwenda mahali pamoja, Soko la Umoja wa Mataifa (www.ungm.org), na kujisajili kufanya biashara na jumuia nzima ya Umoja wa Mataifa. Mara nyingi tunatembelea nchi za bara Afrika kuadaa semina za biashara, na katika semina hizo, tunazungumza kuhusu fursa za kufanya biashara na Umoja wa Mataifa. Pia tunawafundisha watu kuhusu namna ya kujisajili. Katika siku zijazo tutatoa mafunzo kwa watu kuhusu namna ya kujibu mwaliko wa zabuni (ITB) au Ombi la pendekezo (RFP).

Je, mnayo sera ya kulinda mazingira? Kama ipo, mnaitekeleza vipi?

Tangu 2017 tumekuwa na mkakati kuhusu mazingira, haswa kwa operesheni za kulinda amani, na tunao mfumo wa usimamizi wa mazingira. Mfumo huu hushughulika na mambo kama vile nishati, maji, maji taka, taka ngumu, nk. Tunatambua kuwa tunafaa kuwa tumefanya vizuri zaidi katika mambo haya, lakini tumejitolea kuboresha hali katika siku zijazo. Umoja wa Mataifa unafaa kusema na kutenda na wala siyo kusema tu.

Je, una ujumbe kwa vijana wa Afrika, haswa wale wajasiriamali?

Kuna uvumbuzi mwingi sana unaoendelea barani Afrika. Kwa mfano, kuna kompyuta kibao ambayo inaweza kufuatilia mpigo wa moyo wa mtu na kusoma EKG yake [electrogardiogram]na matokeo yanaweza kutumwa kwa daktari ambaye anaweza kuwa umbali wa maili 5,000 kuchambua na kutoa uaguzi. Afrika pia iko kwenye mstari wa mbele katika matumizi ya simu ya mkono kutekeleza majukumu ya benki, nishati ya sola, na usambazaji wa umeme-mbadala. Kwa hivyo, ujumbe wangu kwa vijana ni, "Endeleeni Kuvumbua." Mustakabali wa Afrika unaangaza, hauna kikomo, na ni wa kusisimua mno.

 

Mada: